Angalia hapa unachotakiwa kufanya sasa.
1.Badala ya kuongea kuhusu matukio mabaya na kutokubadilika, ongea kuhusu mambo ya kufurahisha na matukio yalio mazuri. Uwe makini usiruhusu mawazo mabaya yakutawale tena.
Hata kama hakuna mtu anayekusikiliza , ongea mwenyewe.Hakuna tatizo katika hilo. Nimekuwa nikijitania mwenyewe na kucheka ninapokuwa mwenyewe. Wakati ninapokumbuka utani wowote naongea.
Hata unapokuwa unaumwa na unasikia maumivu, fanya utani na kucheka. Uwe unafahamu kuwa unaposikiliza matatizo na maumivu unayafanya yapate nguvu, na kuyafanya yakutawale wewe na maisha yako. Badale yake uwe na usikivu katika mawazo mazuri ya kufurahisha.