Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

852902343_163157.jpg
 
MWANZA: Jeshi la Polisi limemkamata Prosper Lema(26), kwa kosa la kujiteka kisha kutuma ujumbe kwa ndugu zake akitaka atumiwe pesa kiasi cha Tsh. Milioni 5.3, ili aachiwe huru na watekaji - Kamanda wa Polisi, Ahmed Msangi amesema taarifa za Lema zilipatikana baada ya ndugu zake kwenda katika kituo cha Polisi Kirumba kutoa taarifa ya ndugu yao kutekwa na watu wasiojulikana Julai 18, mwaka huu baada ya kuwatumia ujumbe wakiomba fedha - Inadaiwa kuwa Lema alifanya hivyo ili kuongeza mtaji katika biashara yake ya kuuza vileo - Aidha, Msangi ameongeza kwamba mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani pindi uchunguzi wa tukio hilo utakapokamilika.
 
Saini ya Modric ina thamani trillioni 1.9 - Real Madrid : Baada ya kumpoteza Cristiano Ronaldo aliyehamia Juventus, Real Madrid sasa wanaonekana kutokuwa tayari kumpoteza mchezaji mwingine katika kipindi hiki cha usajili. . Wiki hii mwanzoni Inter Milan walionyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji bora wa kombe la dunia 2018 - Luka Modric. . Baada ya kutoka kwa ripoti hiyo, leo Raisi wa Real Madrid, Florentino Perez amesema kwamba klabu yoyote inayomhitaji Modric itabidi iwalipe kiasi cha trillioni 1.9 - sawa na €750m.
 
Mwezi mmoja uliopita wakati Uingereza ilipokuwa ikiwania kufika nusu fainali ya kombe la dunia, huku timu kuu zikijiandaa kwa msimu mpya, mechi ya mwisho ya Manchester United dhidi ya Real Madrid ilikumbwa na maswali chungu nzima.
Gareth Bale atachezeshwa lakini atamchezea nani? Mbali na maandalizi ya msimu huu, hatahivyo Bale sasa anafuraha chungu nzima baada ya mkufunzi mpya wa klabu hiyo Julen Lopetegui kumhakikishia kwamba atamshirikisha katika kikosi chake.
 
Na huku Man United ikijianda kwa mechi ya siku ya Jumatano , maswali mengi juu ya United bado yanasalia.
Matamshi ya mkufunzi Jose Mourinho katika uwanja wa Michigan nchini Marekani siku ya Jumamosi wakati kikosi chake kilipopoteza 4-1 yalikuwa na uzito mkubwa.
Hivyobasi ni wakati wa kuuliza maswali haya.
Ni nini kinachoendelea na Mourinho na Manchester United?
 
Kwa nini Mourinho hana raha tena?
Mbele ya kamera ,Mourinho amekuwa mtu ambaye hana raha kwa muda mrefu sasa. Kitu, makovu ya kukabiliana na vyombo vya habari vya Uhispania wakati akiifunza Real madrid yalitokea wakati akiifunza Chelsea mara ya kwanza na mara ya pili.
Chochote kile , Mourinho amebadilika na kuwa mkufunzi ambaye motisha yake imeshuka katika klabu hiyo.
Hatahivyo malalamishi aliyotoa baada ya mechi dhidi ya Liverpool yanaonyesha kocha aliyeshushwa mabega.
 
Alilalama kuhusu ukosefu wa wachezaji nyota, kiwango cha baadhi ya wachezaji wadogo mbali na kuzungumzia kuhusu malengo yake ya wachezaji wapya ambayo anaona hayataafikiwa , akisema kwamba baadhi ya wachezaji wake wanahudumia majeraha, akawomba wachezaji nyota kurudi matika mazoezi mapema na akahoji ni kwa nini mashabiki wanalipa ili kuona timu yake ikicheza.
Katika mkutano wake na vyombo vya habari uliochapishwa sana na kutangazwa, alimshukuru beki Eric Baily kwa kuingia na kuchukua mahala pake Chris Smalling wikendi, na baadaye kumkashifu raia huyo wa Ivory Coast kukosa uongozi.
 
Akizungumza na runinga ya United , alimshutumu nahodha mpya Antonio Valencia kwa kurudi kutoka likizo na kiwango cha chini cha mchezo.
Akiongezea , alishutumu kiwango cha refa ambaye alitoa penalti mbili dhidi ya timu yake.
La muhimu ni je Mourinho ameanza kukasirishwa na mambo haya yote , je anajaribu kuwasilisha picha fulani?
Ama anatafuta sababu za kujiondoa katika lawama baada ya kushindwa vibaya na wapinzani wake katika ligi ya Uingereza Liverpool?
Iwapo sio hayo yote basi ni miongoni mwa mbinu za ukufunzi wake ama anataka kuondoka baada ya miaka mitatu swali ambalo hulikataa kwa haraka anapoulizwa.
 
Je uhusiano wake na klabu hiyo umeharibika?
Kuna majibu mawili ya kile ambacho Mourinho alikifanya siku ya Jumamosi. Mwanzo mtu atajiuliza maswali, na kusema ni tabia yake ama amuonee huruma na hali yake na kusahau.
Hiki ndicho kinachofanywa na idadi kubwa ya viongozi wa klabu hiyo. Hatahivyo raia huyo wa Ureno alitia saini kandarasi mpya mnamo mwezi Januari ambayo iliimarisha mahitaji yake ya kikazi mbali na kumuongezea kandarasi yake hadi mwaka 2020.
 
Uhusiano kati ya Mourinho na naibu mwenyekiti wake Ed Woodward umesemekana kuwa mzuri sana kati ya wote wawili hivyobasi mpango wowote wa kuwanunua wachezaji wapya ungejadiliwa na kuafikiwa katika mazungumzo yao.
Hivyobasi ni nini ambacho kimebadilika baada ya kukosa kumsajili mchezaji mmoja- swala ambalo limekuwepo misimu miwili iliopita? hayo ni maoni mbadala, na kuna wakuu wengine ambao wameanza kulemea upande huo, je Mourinho anataka kuondoka na huu ndio mpango wa kutaka kujitoa.
 
Back
Top Bottom