USHAWAHI kuwaza kutokelezea huku ukiwa umejitupia suruali aina ya jeans na koti yenye mtindo tofauti? Basi leo ngoja tuone ni vipi unaweza kuvaa jeans yako tight na koti katika sehemu mbalimbali.
Aina hii ya nguo yani si ya kuikosa katika kabati lako. Kwani ni rahisi sana kuistyle na kuendana na mazingira unayotaka kwenda. Mfano mzuri aina hii waweza kuivaa katika eneo lako la kazi, wengi wetu tumekariri jeans ivaliwe siku za wikiendi mfano Ijumaa, lakini ukivaa jeans yako hii na kuitafutia top matata sana na kunogesha mwonekano wako na koti la ukweli.