Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Chelsea na Man City zinakutana kwenye Uwanja wa Wembley katika mpambano mmoja matata wa kukata utepe wa Ligi Kuu England.

Mchezo huo wa kuwania Ngao ya Jamii, tayari umewajenga hofu makocha wa pande zote, Maurizio Sari wa Chelsea na Pep Guardiola wa Man City.

Kocha wa City, Guardiola anaonekana kuficha kikosi chake huku mwenzake, Sarri, akiita wasaidizi wake wote na kufanya kikao kilichotumia zaidi ya saa tatu.
 
Sarri aambaye amemrithi mtaliano mwenzake Antonio Conte, tangu atue hapo hajawahi kukutana na wasaidizi wake wote kwa pamoja, hivyo hii ni mara ya kwanza kufanya hivyo,na walijichimbia makao makuu ya klabu hiyo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge wakijadili namna ya kuikabili City katika mchezo huo.

Katika kikao hicho kilichoongozwa na Sarri mwenyewe, kiliwajumuisha wasaidizi wake, wakiwemo wathamini wa mechi, watalaamu wa viungo, makocha wasaidizi, makocha wa makipa na madaktari.
 
Sehemu kubwa ya wasaidizi hao ni wachezaji wa zamani wa Chelsea ambao ni, Gianni Picchioni, Massimo Nensi, Davide Losi, Davide Ranzato, Marco Ianni, Gianfranco Zola, Paolo Bertelli, Henrique Hilario, Luca Gotti na Carlo Cudicini.

Kikao hicho kichofanyika juzi usiku, lakini kilichojadiliwa hakikuwekwa kwenye mtandao wa Chelsea, jambo linalodhihirisha kuwa kilikuwa cha ajenda maalumu kuhusiana na mechi hiyo.
 
Sarri atamuanzisha kiungo aliyemsajili baada tu ya kutua Chelsea, Jorginho na katika wachezaji wa kikosi cha kwanza atakaowakosa ni wale waliotarajiwa kuondoka, Eden Hazard na kipa Thibaut Courtois ambao walichelewa kujiunga na wenzao baada ya kumalizika fainali za Kombe la Dunia. Majeruhi pekee ni Cesc Fabregas aliyeumia dhidi ya Arsenal, Jumatano wiki hii.

Wakati Sarri akiingiwa na hofu, mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich, atakuwepo uwanjani na amemwambia hatojali matokeo, bali anataka kuona soka linalovutia la pasi safi.
 
Mshambuliaji chiupukizi wa Ufaransa, Ousmane Dembele, 21, ameonekana kuligwaya benchi kwenye timu yake ya Barcelona.

Chipukizi huyo wa Ufaransa ammbaye alihamia Barcelona mwaka jana, ameshacheza mechi 17 na kufunga mabao matatu lakini hana uhakika wa namba.

Kutokana na hilo mshambuliaji huyo alitumia kipindi cha mapumziko baada ya fainali za Kombe la Dunia kuteta na marafiki zake wanaokipiga katika Ligi Kuu England kuulizia timu ambayo atakuwa na uhakika wa namba.
 
Ingawa marafiki zake wengi aliokua akizungumza nao ni wachezaji wa Arsenal, lakini amebainisha kuwa hafikirii kujiunga na timu hiyo ya Kaskazini mwa jiji la London.

Amesema anafikiria kwenda timu ambayo atakuwa na uhakika wa kucheza kila mechi ili kulinda kipaji chake kabla ya kutua Barcelona, Dembele aliichezea Borussia Dortmund ya Ujerumani ambako aling’ara.

Katika msimu mmoja aliocheza akiwa mshambuliaji msaidizi alifunga mabao sita katika mechi 32 alizocheza jambo lililoivutia Barcelona na kumsajili.
 
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema atawatumia wachezaji saba wasio wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya kuikabili Chelsea mechi ya Ngao ya Jamii leo Jumapili kwenye dimba la Wembley.

Hata hivyo hakuwataja kabla ya taarifa kufichuka kuwa ameteta na wachezaji wake wote kuwasihi wasahau uchovu badala yake wapiganie ushindi katika mchezo huo.
 
Wachezaji pekee ambao imethibitika kuwa hawatajumuishwa kwa kuwa hawajafanya mazoezini na wenzao ni Kevin De Bruyne na Raheem Sterling, lakini wengine wote wapo na inaaminika anaraka kuwahadaa Chelsea ili wapange kikosi dhaifu na yeye ashushe jeshi lake kamili.

Imebainika kuwa kati ya wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao walicheza fainali za Kombe la Dunia 2018 na wanatarajiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha leo ni pamoja na Benjamin Mendy, John Stone, Kyle Walker, Vincent Kompany na Fabian Delph. Mchezaji pekee aliyesajiliwa na City kutoka Leicester City, Riyad Mahrez anatarajiwa kuwepo kikosini ingawa aliumia dhidi ya Bayern Munich.
 
Aisee..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…