Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Michael Oliver - Newcastle United

Mwamuzi Oliver anatokea katika Mji wa Ashington. Kwenye Ligi Kuu England aliingia mwaka 2010. Msimu uliopita alichezesha fainali ya Kombe la FA, ambapo Chelsea iliichapa Manchester United 1-0. Oliver, aliyezaliwa Februari 20, 1985 rekodi zake zinaonyesha amechezesha mechi 203, akitoa kadi za njano 656 na nyekundu 28. Mwamuzi huyo anashabikia Newcastle United.
 
Jon Moss - Sunderland

Mwamuzi Moss, anatokea kwenye Mji wa Sunderland na ndiyo maana haishangazi kuona amekuwa shabiki wa Sunderland. Mwamuzi huyo aliingia kwenye Ligi Kuu England mwaka 2011 na mechi yake kubwa kuchezesha ilikuwa fainali ya Kombe la FA mwaka 2015, ambapo Arsenal iliichapa Aston Villa.

Rekodi za Moss, aliyezaliwa Oktoba 18, 1970 amechezesha mechi 173, ametoka kadi za njano 584 na nyekundu 25.
 
Andre Marriner - Aston Villa

Mwamuzi Marriner anatokea Mji wa Birmingham na timu yake anayoshabikia ni Aston Villa.

Refa huyo aliingia kwenye Ligi Kuu England mwkaa 2005, huku mechi yake kubwa aliyochezesha ikiwa ni fainali ya Kombe la FA mwaka 2013, ambapo Wigan iliichapa Manchester City 1-0. Rekodi zake Marriner amechezesha mechi 282, ametoa kadi za njano 911 na nyekundu 52.
 
Kevin Friend - Leicester City

Kevin Friend anatokea Mji wa Tottenham, lakini timu anazoshangilia ni mbili, Leicester City na Bristol City.

Mwamuzi huyo aliyezaliwa Julai 6, 1971 aliingia kwenye Ligi Kuu England mwaka 2009 na rekodi zake zinaonyesha amechezesha mechi 178, akitoa kadi za njano 629 na nyekundu 20.
 
Anthony Taylor - Altrincham

Mwamuzi Taylor anatokea kwenye Mji wa Manchester, lakini klabu anayoshabikia si Man United wala Man City, bali ni Altrincham.

Taylor, aliyezaliwa Oktoba 20, 1978 aliingia kwenye Ligi Kuu England mwaka 2010 na rekodi zake zinaonyesha amechezesha mechi 193, ametoa kadi za njano 662 na nyekundu 30.
 
Back
Top Bottom