Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Atachukua mahala pake Mblegiji Thibaut Courtois ambaye anaamini kuwa kukataa kwake kurejea Chelsea kufanya mazoezi kutalipwa na kuhamia Real Madrid. Klabu hiyo ya Uhispnaia unajiandaa kumruhusu kiungo wa kati raia wa Croatia Mateo Kovacic, 24, kuelekea Stanford Bridge kwa mkopo kama sehemu ya mkataba huo. (Daily Telegraph)
 
Tottenham walitoa ofa ya pauni milioni 25 kwa mchezaji za zamani raia wa England kikosi cha chini ya miaka 21 Jack Grealish, 22, siku ya Jumanne na wanasubiri jibu kutoka kwa Aston Villa. (Telegraph)
 
West Ham wakati huo huo wana matumaini ya kukamilisha makubaliano ya pauni milioni 5 kumsaini mshambuliaji wa Asenal raia wa Uhispania mwenye miaka 29 Lucas Pezer ndani ya saa 24 zinazokuja. (London Evening Standard)
 
Kipa wa England Jack Butland atalazimika kubaki Stoke City kwa sababu kumsainiaatakayechukua mahala pake itakuwa vigumu kwa kuwa tarehe ya mwisho inakaribia, kwa mujibu wa meneja wa Potters Gary Rowett. (Sentinel)
 
Chelsea imekubali kumuuza mlinda mlango wake raia wa Ubelgiji Thibaut Courtois Real Madrid huku ikihitaji nyongeza ya kiungoo Mateo Kovacic kwa mkopo wa muda mrefu.
Chelsea inasema makubaliano hayo yanasubiri mazungumzo ya mwingo baina ya Courtois na Real Madrid sambamba na vipimo vya afya.
Madrid inatarajia kukamilisha usajili wa Courtois ambaye aliibuka mlinda mlango bora kwenye kombe la dunia kabla ya muda wa usajili kufikia kikomo Alhamisi.
 
Mlinda mlango wa Athletic Bilbao Kepa Arrizabalaga, anatarajiwa kuziba pengo ndani ya Chelsea kwa ada ya Paundi milioni 71, hii ikiwa ni rekodi mpya na ya juu zaidi kwa nafasi hiyo.
Kiungo wa Croatia Kovacic, 24, atafanyiwa vipimo vya afya siku ya Jumatano kabla ya kujiunga na miamba hiyo ya London kwa mkopo wa muda mrefu.
 
Courtois amekua mchezaji wa Chelsea tokea mwaka 2011 alipojiunga nayo akitokea Genk.
Alielekea Atletico Madrid kwa mkopo mpaka mwaka 2014 aliporejea darajani kama mchezaji namba moja katika nafasi ya mlinda mlango.
Alikosekana katika mazoezi siku ya Jumatatu baada ya kuwa mapumzikoni kufuatia kushriki kombe la dunia.
 
Kepa, 23, anatarajiwa kuwasili Stamford Bridge huku akiufunika usajili wa mlinda mlango mpya wa Liverpool Alisson aliyejiunga kwa ada ya Paundi Milioni 66 tokea Roma.
Ni mlinda mlango namba mbili kwenye timu ya taifa ya Hispania akiwa nyuma ya David de Gea wa Manchester United huku akicheza mpambano mmoja wa kimataifa
 
Zinaweza kuwa ni habari zitakazowashtua mashabiki wa Arsenal au zisiwashtue kwa sababu pengine klabu haitabadilika kwa kiwango cha wagusa moja kwa moja mashabiki. Arsenal muda wowote kuanzia sasa inaweza kuwa mikononi mwa mtu mmoja kwa asilimia 100. Imefichuka kuwa kampuni Kroenke Sports&Entertainment chini ya bosi wake Stan Kroenke ipo tayari kuzinunua hisa zote zilizokuwa zikimilikiwa na tajiri Alisher Usmanov.
 
Kampuni hiyo kutoka nchini Marekani ambao ndiyo wamiliki ndiyo wamiliki wakuu wa Arsenal wameshaweka tayari kitika cha dola za Kimarekani bilioni 1.8 kwa ajili ya kubeba asilimia 100 ya hisa zote za Arsenal.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…