Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

SI unajua Jumapili ya leo kuna kile kipute matata huko Emirates kati ya Arsenal na Manchester City kwenye Ligi Kuu England, basi bana kocha Unai Emery ameshafahamu atatokajetokaje kwenye mechi hiyo.

Kocha huyo mpya huko Arsenal, Emery ambaye ameanza ujanja ujanja kwa kusema kwamba Pep Guardiola ni bora kuliko yeye, ataingia uwanjani na fomesheni ya 4-2-3-1.

Hata hivyo, kama utakuwa umemkariri Emery kwa fomesheni hiyo pekee, basi itakula kwako, kwani kikosi chake kitabadilika kwa kadri mechi inayokwenda na wakati mwingine ndani ya uwanja wataonekana wakiwa kwenye mtindo wa 4-3-3.
 
Kikosi ambacho kinatajwa kwamba kinaweza kuanzishwa kwenye kuwavaa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England, Man City, golini kutakuwa na mabadiliko makubwa, ambapo kipa mpya Bernd Leno ataanza mbele ya Petr Cech, huku kwenye safu ya mabeki kukitarajiwa kuwapo na Hector Bellerin, Sokratis Papastathopoulos, Shkodran Mustafi na Ainsley Maitland-Niles.

Kwenye safu ya kiungo, kutakuwa na Lucas Torreira, Granit Xhaka na Aaron Ramsey, huku kwenye fowadi kutakuwa na wakati Mesut Ozil, Henrikh Mkhitaryan na Pierre-Emerick Aubameyang.
 
Ninasikitika kuona ninahusishwa na kuwa Kocha wa Argentina, bahati mbaya mimi sijazungumza na yeyote kati ya viongozi wa Chama cha soka, nashangaa mmoja kati ya viongozi amesema wanashindwa kunifuata kwa kuwa mimi nitahitaji fedha nyingi za mshahara tuseme wao wanajua mshahara ninaolipwa hapa?,” alihoji Guardiola.

Kocha huyo yupo katika mwaka wa tatu wa kuinoa Man City, akiwa tayari ameipa ubingwa wa Ligi Kuu England na kuifikisha katika robo fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya ambayo ni hatua ya juu kabisa kufikia na timu hiyo.
Mbona man city walifika hadi semi final mkuu.
 
Mwigizaji mahiri na mwanamuziki nyota duniani, Jennifer Lopez ‘J Lo’, mwenye miaka 49, amenunua jumba lingine la kifahari eneo la Bel Air, Los Angeles, Marekani.

J Lo ambaye analo jumba kubwa, ameamua kuongeza jumba jingine jijini Los Angeles, ingawa anaendelea kusaka wateja wa kuinunua nyumba yake nyingine iliyopo eneo la California kwa Pauni 12.5 milioni.

Mwanamuziki huyu anayeingiza kipato kikubwa anaonekana kuchanganywa na kipato kwani jumba alilolinunua sasa lina uwanja wa ziada wa ekari nane, jumba hilo liliwekwa sokoni kwa Pauni 40 milioni lakini yeye alitoa ofa ya kununua kwa Pauni 28 milioni
 
J Lo alilinunua jumba hilo mwaka 2010 akiwa na mumewe mwimbaji Marc Anthony kwa Pauni 8.2 milioni, awali aliiweka sokoni kwa Pauni 17 milioni, lakini ikakosa mteja.

Septemba mwaka huu J Lo aliamua kupunguza bei na kuiuza kwa Pauni 14.5 milioni hata hivyo hakuna mteja aliyepatikana hivyo sasa anaiuza kwa Pauni 12.5 milioni.
 
Back
Top Bottom