Unajua unaponunua gesi ni tofauti na mkaa au kuni, mkaa unanunua Sh1,500 au Sh2,000 kwa siku, sawa ni kubwa ukijumlisha kwa mwezi lakini unapotaka kununua gesi ni lazima uwe na fedha taslimu 21,000 ndipo upewe, nitaweza wapi wakati mimi maisha yangu ya kuunga unga,” anasema Rose.
Kauli ya Rose inaungwa mkono na muuzaji wa gesi ya kupikia katika eneo la Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam, Yohana Charles anasema licha ya kuwa uingizwaji wa gesi ya kupikia nchini umeongezeka, gharama za uuzaji wa gesi hiyo bado uko juu.