WAKATI mwingine anaweza akakanyagwa vibaya hapo labda hata maeneo ya jicho na kuumia lakini ukamuona anaendelea kucheka na kumuacha mwanae aendelee na kile anachokifanya.
Sio kwamba anakuwa hajasikia maumivu...hapana huenda naumivu kayasikia sana lakini maumivu yale hujikuta yamefunikwa na furaha ya kumuona mwanae anatabasamu na kufurahia kile anachokifanya,kuvumilia kote kule ni kwasababu tu ya kutaka kumuona mwanae anafuraha.
Ndio maana hata leo ukikutana na mtu yoyote ukamuuliza unapenda nani zaidi kati ya mama au baba yako bila kusita wala kuumiza kichwa hata kabla hujamaliza kuongea atakujibu nampenda zaidi MAMA,sio kwamba mtu huyu hampendi na baba pia,hapana anampenda lakini mama zaidi kwasababu Wamama siku zote humimina upendo wao kwa asilimia 100 kwa wanao wakati wowote ule,haijarishi mtoto ni mkubwa vipi na haijarishi anapitia maumivu yapi lakini upendo wa mama kwa Mama kwa mtoto huwa unabaki pale pale.
Ukitaka kushuhudia harufu ya kibao kikali hapo mtoto huyo ahamie kwa Baba na kuanza kumkanyaga hivyo,ndugu yangu utamshuhudia Mama huyo akimuokota mwanae chini ya uvungu akilia.Mungu awabariki sana Wanawake wote kwa uzao na malezi yenu mema.