Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

*MCHUNGAJI MWIZI?*

Wanandoa walimualika MCHUNGAJI nyumbani kwao wakati wa sikukuu ya Pasaka.

Baada ya MCHUNGAJI kula na kuondoka, Mke alimwambia mumewe kuwa sh 10000 aliyokuwa ameiweka mezani imetoweka. Wakaisaka bila mafanikio na kushuku kuwa huenda Mchungaji ndio ameiba na kuondoka nayo.

Jambo ambalo liliwakera sana kuona Mchungaji anaiba.

Baada ya mwaka mmoja Pasaka nyengine kuingia, wanandoa kama ilivyo kawaida yao wakamualika tena Mchungaji wao ambaye alikuja kuwa ni yule yule na safari hii akiambatana wasaidizi wake pamoja na Mchungaji mgeni ambaye ni mpya kwenye eneo lao kwa lengo la kumtambulisha kwao.

Hata hivyo Kwa jinsi tukio la Pasaka iliyopita lilivyowakera, wakaamua kumuuliza Mchungaji mbele ya wageni wote kama iwapo alichukua noti ya sh.10,000/- yao mwaka uliopita.

Mchungaji alishtuka na kwa masikitiko akajibu "La Hasha sikuchukua ile noti.

Bali nilichokifanya niligundua nyumba hii hamna mazoea ya kusoma Biblia nikaweka hiyo noti ya sh. 10,000/- ndani ya BIBLIA iliyokuwa mezani, na nikaongeza noti zingine mbili zangu kama zawadi kwenu."

Mchungaji akaenda kuchukuwa Bblia iliyokuwa imehamishwa juu ya TV[emoji342] na kuzikuta pesa ziko vile vile kama alivyoziweka.

Mchungaji akasema; "MUNGU wangu"[emoji86][emoji134]‍♂[emoji134]‍♀, ina maana kati yenu hakuna aliyefungua Biblia kuisoma katika kipindi chote cha mwaka mzima? Mnaipuuza hazina kuu ambayo ni Biblia Neno la MUNGU?"

*Wanandoa wakatahayari na kuisikitikia aibu yao....................*

JIULIZE NAWE UMEWASAIDIA WANGAPI KUSOMA BIBLIA???


Shukran!
 
IMG_20180816_204205_050.JPG
 
Kocha wa Arsenal, Maurizio Sarri amepangua kila utaratibu uliowekwa kwa wachezaji na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Antonio Conte.

Sarri alianzia kwenye chakula wakati wa kujiandaa na mchezo, alisema kuwa kila mchezaji atakula kulingana nanavyodhani inafaa kwa ajili ya mchezo.

Conte alikuwa mkali kwenye suala la kula ovyo Stamford Bridge na amekuwa akipanga nini mchezaji anatakiwa kula, kipindi chote alichokuwa klabuni hapo.
 
Sarri pia ametaka wachezaji wa Chelsea kutolala pamoja hotelini siku moja kabla ya mchezo Stamford Bridge, utaratibu ambao hata hivyo bado ulikuwa mgumu kutekelezeka.



gazeti la Daily Telegraph lilisema kuwa Sarri amelegheza utaratibu wa kula kwa wachezaji na wachezaji wameambiwa kula wanachotaka lakini kwa mpangilio.



Sarri amefuta mpango aliouanzisha Conte wa kulala hotelini siku ya mechi, lakini mpango mpya ni kwamba hata siku ya mechi hakuna mpango wa kulala hotelini na wachezaji watatoka nyumbani na wanakutana klabuni tayari kwa mchezo.
 
Back
Top Bottom