Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema anatarajiwa wachezaji wataondoka katika klabu hiyo kabla ya kufika muda wa mwisho wa uhamisho wa wachezaji Ulaya licha ya kuwa timu hiyo haikusajili mchezaji yoyote msiu huu wa joto.(Sky Sports)
 
Newcastle italazimika kulipa kitita cha fedha iwapo itaamua kumsajili mshambuliaji wa Venezuelan Salomon Rondon, mwenye miaka 28, katika mkataba wa kudumu msimu ujao wa joto baada ya West Brom kuidhinisha kuongeza kwa mwaka mmoja mkataba wake. (Sun)
 
Mchezaji wa kushoto wa Manchester City Oleksandr Zinchenko huenda anakaribia kuhamishwa kwa mkopo kuelekea Real Betis au Girona baada ya mchezaji huyo wa miaka 21 kukataa ombi la kuhama kabisa kwenda Wolves msimu huu wa joto. (Mirror)
 
Barani Africa leo nyasi za viwanja vinne zitawaka moto katika michezo ya hatua ya makundi ya klabu bingwa.
Vinara wa kundi A Espérance Sportive de Tunis ya Tunisia watakuwa wenyeji wa Al Ahly kutoka nchi Misri
Katika kundi B, Entente Sportive de Sétif ya Algeria watakuwa katika dimbani kuwakabili TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemocracy ya Congo.Ambayo tayari zimejihakishia kusonga mbele wakiwa na alama 10 mkononi.
 
Back
Top Bottom