Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Amen. Mimi ni mmojawapo.
Kuna member ali comment kwa kumtaja rafiki yake aliye kuwa anaumwa kama mleta uzi, cha zaidi kataja umri na shule.
Hizi Id zinaficha mengi sana, alizikwa hapa Kibaha mchana,alikuwa na wadhifa na mtu wa watu sana....
Aisee. Apumzike kwa amani. Maisha yetu haya basi tu...
 
Aisee. Apumzike kwa amani. Maisha yetu haya basi tu...
Hata sijui nakosea wapi! Natamani nife nikiwa na amani, nife sura ikiwa ina nuru.

Jamaa zake wa karibu wanasema mpaka anakata roho alikuwa anatabasamu. He was happy at the end. Kuna funzo kubwa sana... Natamani nipate darasa toka kwako mkuu. Kufa kupo, hakukwepeki
 
[emoji124] [emoji124] [emoji124] Yeye hajui kuwa kuna mizigo mingine utadhani ina miiba... Hata style ya kuibeba inakuwa taabu kuipatiaView attachment 839498
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] sasa tunda kama hili hapa na miba zake, jamaa wanabebaga tu[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
FB_IMG_1530632738174.jpg
 
HEKIMA ZA BABU KIPOFU

Babu mmoja kipofu aliishi katika nyumba ndogo peke yake...lakini majirani walimsaidia chakula kumfulia nguo na mambo madogomadogo...

Kijana mmoja alikuwa na kazi ya kumuwashia taa. Kila jioni alikwenda kwa babu kuwasha taa ya chemli na kuondoka.

Siku moja kijana alipokuwa anawasha taa ya babu...kijana akasema "babu hii taa ninayokuwashia inakusaidia nini na wewe huoni? Naona unamaliza pesa kununua mafuta ya taa kila siku..."

Babu akamjibu kijana.
"Aah...ni kweli mjukuu wangu, asante kwa kunizindua nimekuwa mjinga miaka mingi kuwasha taa ilhali hainisaidii...basi wacha usiwashe tena"
Kijana akafurahi kuona ushauri wake umefuatwa hakuwasha taa...akamuaga babu anaondoka huku nyumba ya babu ikiwa na kiza totoro.

Mara kijana kabla hajatoka mlango wa babu akajikwaa akaanguka, babu akasikia kishindo kilichoambatana na yowe la kijana....babu akahamaki akauliza "kuna nini?"

Kijana akajibu angali makalio yapo sakafuni....
"babu nimejikwaa na kigoda chako"

Babu akauliza kwa istihzai...
"mjukuu wangu nawe umekuwa kipofu huoni kama mimi? "

Kijana akasema....
"hapana babu wakati natoka kulikuwa na giza sikuweza kuona kigoda nikajikwaa"

Babu akacheka sana kiasi cha kumshangaza kijana babu anacheka nini?

Akamuuliza
"babu badala ya kunipa pole unanicheka kulikoni?"

Babu akajibu...
"Nilipokuwa nikikuita uniwashie taa haikuwa kwa ajili yangu. Ni kwa ajili yenu nyinyi mnaoona mkija kunisalimia msijikwae. Kadhalika hata ukiona mtu ameoga ametakata amejipulizia manukatato sio kwa ajili yake tu Bali kwa ajili ya furaha ya wenzake. Asiwanukize jasho na kuwaudhi..
Sasa Niwashie taa uende zako.
Kijana akawasha taa na kuondoka
 
Back
Top Bottom