Mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud, amehakikishiwa na Kocha Maurizio Sarri, kuwa ataanza katika kikosi kitakachocheza kesho dhidi ya timu yake ya zamani ya Arenal.
Mchezo huo wa Ligi Kuu England, utachezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge na Kocha Sarri kwa makusudi kabisa amempa nafasi akiamini anawajua vilivyo Arsenal hivyo itakuwa rahisi kwake kuwaadhibu.
Maurizio Sarri, alisema kuwa anapenda kumtumia mshambuliaji huyo kutokana na uwezo wake wa kuwasumbua mabeki wa timu pinzani na anaamini aaifunga Arsenal.