Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan ameaga dunia akiwa na miaka 80.
Annan alikuwa ni mwafrika mweusi wa kwanza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, akihudumu mihula miwili kuanzia mwaka 1997 hadi 2006.
Baadaye akahudumu kama mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria na kuchangia kupatikana kwa suluhu la amani la mzozo wa nchi hiyo.