Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bosi wa zamani wa vilabu vya Everton, Manchester United, Sunderland na West Ham David Moyes anaongoza mbio za kupewa nafasi ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Marekani (Sunday Times - subscription only
 
Manchester City wameambiwa watalazimika kuilipa Borussia Dortmund's kiasi cha pauni milioni 68, kama inataka kumsajili kiungo Julian Weigl, ambae pia anawindwa na miamba ya soka ya Ufaransa Paris St-Germain (France Football, via Sun on Sunday)
 
Chelsea iko tayari kusikiliza ofa itayokuja klabuni hapo ikimtaka mchezaji wa kiungo Danny Drinkwater, ambae ameanza katika michezo mitano tu ya msimu uliopita akiwa amesajiliwa kwa kiasi cha pauni 35 akitokea Leicester City (Mail on Sunday)
 
Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amejitetea kufungwa na Brighton si kwamba hana mawasiliano na wachezaji wake.

Pamoja na Alexis Sanchez kukosekana kutokana na kuwa majeruhi, kikosi cha Man United kilikuwa kimekamilika waliposafiri kuifuata timu hiyo, ambayo iliwaadhibu kwa kutumia makosa ya mabeki wao.

Victor Lindelof na Eric Bailly walifanya makosa kwa kuchanganyana kiasi cha kusababisha vijana wa Chris Hughton akienda wavuni mara tatu kabla ya Paul Pogba kuifungia penalti United dakika za lalasalama.

Alipoulizwa kama kulikuwa na tatizo la mawasiliano kati yake na wachezaji wake, Mourinho alijibu kwa hasira akisema: ‘Inatakiwa ufahamu tofauti na zaidi kuangalia nini kimetoea uwanjani kati ya wachezaji. ‘Tumefanya makosa na tumefungwa kimakosa, hayo naweza kuyasema.’

Beki wa zamani wa United, Gary Neville, alishindwa kujipanga na akizungumzia kipindi cha kwanza hasa beki wa kati wa United kwa jinsi walivyokuwa wakicheza. ‘Kuna mabeki wa kati watano katika klabu. Kuna pea ambayo unaweza kuiamini na kukupeleka kwenye ubingwa?

Swali kwa Jose [Mourinho] linahitaji majibu,’ Neville aliiambia Sky Sports. ‘ Kila beki wa United…hawajatulia, wanashambulia lakini wakati mwingine hawafanyi. ‘ Bailly alifanya ovyo, ovyo sana.

Jose amechukizwa na kile alichokiona. Yote [ngome] kila mmoja alicheza ovyo. Alichukizwa sana. ‘Ndivyo inavyokuwa wakati mambo hayaendi. Makosa katika ngome.
 
Kiungo Luka Modric, Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah wameingia katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mwanasoka bora mwaka wa Uefa.

Kiungo wa Real Madrid, Modric, na mshambuliaji mpya wa Juventus, Ronaldo pamoja na mshambuliaji wa Liverpool, Salah ndiyo watakaopigiwa kura na makocha 80 na wanahabari 55.

Tuzo hiyo itatolewa Agosti 30, wakati wa upangaji wa makundi ya Ligi ya Mabingwa jijini Monaco.

Ronaldo, alijiunga na Juventus akitokea Real Madrid kwa gharama ya pauni99.2milioni Julai, alishinda tuzo hiyo mwaka 2017.

Wanaowania tuzo hiyo kwa wanawake ni pamoja na Pernille Harder, Ada Hegerberg na Amandine Henry.
 
Mshambuliaji mahiri wa Wales, Gareth Bale jana alivaa rasmi viatu vya Cristiano Ronaldo alipotoa pasi ya bao na baadaye kufunga la pili Real Madrid ikiichapa Getafe kwa mabao 2-0, katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Hispania.

Katika mchezo huo wa kwanza kwa Madrid bila Ronaldo, aliyeuzwa kwa Juventus, Bale alijituma na kuhaha kila mahali uwanjani kusaka mabao na krosi yake iliwekwa kimiani na Dani Carvajal dakika ya 20 kuipa Real bao la kuongoza.

Mshambuliaji huyo sasa amehamishiwa kucheza katikati badala ya wingi, alishirikiana vizuri na Marco Asensio na Karim Benzema na juhudi zake zilimuwezesha kufunga bao la pili dakika ya 50.

Kocha mpya wa Real Madrid, Julen Lopetegui ameamua kutumia mfumo wa washambuliaji watatu, tofauti na ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Zinedine Zidane aliyekuwa akitumia washambuliaji wawili.

Uamuzi wa Lopetegui kuwaanzisha Bale, Benzema na Ansensio mbele ulikuwa na manufaa kwani walilishambulia mno lango la Getafe na kama sio umahiri wa kipa David Soria, wangevuna idadi kubwa ya mabao.

Jumatano wiki iliyopota Real ilishindwa kutamba baada ya kufungwa mabao 4-2 na Atletico Madrid, katika mchezo wa Uefa Super Cup na wengi wakadhani Real itaanza vibaya pia Ligi Kuu.
 
AGOSTI 31 ndio itakuwa mwisho wa usajili kwa ligi nyingi za huko Ulaya. England wao walimaliza kusajili tangu Agosti 9 na Italia walifunga usajili wao juzi tu hapo.

Wakati wa majira haya ya usajili wa majira ya kiangazi huko Ulaya, kuna majina ya mastaa 50 yalihusika kwenye mchakamchaka huo, ambapo wengine walihama timu zao na kuwa na timu mpya kwa sasa na wengine bado wakibaki kwenye timu zao za zamani. Haya ndio majina ya masupastaa 50 ambao wametajwa kwenye dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi wakihusishwa na klabu moja kwenda nyingine na baadhi yao wamehama na wengine wamebaki.
 
1.Toby Alderweireld

Timu: Tottenham

Nafasi: Beki wa kati

2.Leon Bailey

Timu: Bayer Leverkusen

Nafasi: Mshambuliaji

3.Gareth Bale

Timu: Real Madrid

Nafasi: Mshambuliaji

4.Michy Batshuayi

Timu: Chelsea

Nafasi: Mshambuliaji

5.Hector Bellerin

Timu: Arsenal

Nafasi: Beki wa kulia

6.Andrea Belotti

Timu: Torino

Nafasi: Mshambuliaji

7.Leonardo Bonucci

Timu: Juventus

Nafasi: Beki wa kati

8.Julian Brandt

Timu: Bayer Leverkusen
 
Nafasi: Kiungo wa kati

9.Marcelo Brozovic

Timu: Inter Milan

Nafasi: Kiungo mkabaji

10.Mattia Caldara

Timu: AC Milan

Nafasi: Beki wa kati

11.Thibaut Courtois

Timu: Real Madrid

Nafasi: Kipa

12.Matteo Darmian

Timu: Man United

Nafasi: Beki wa pembeni

13.David de Gea

Timu: Man United

Nafasi: Kipa

14.Matthijs de Ligt

Timu: Ajax

Nafasi: Beki

15.Lucas Digne

Timu: Everton

Nafasi: Beki

16.Gianluigi Donnarumma

Timu: AC Milan
 
Nafasi: Kipa

17.Christian Eriksen

Timu: Tottenham

Nafasi: Kiungo

18.Nabil Fekir

Timu: Lyon

Nafasi: Kiungo

19.Olivier Giroud

Timu: Chelsea

Nafasi: Mshambuliaji

20.Andre Gomes

Timu: Barcelona

Nafasi: Kiungo

21.Eden Hazard

Timu: Chelsea

Nafasi: Kiungo

22.Gonzalo Higuain

Timu: AC Milan

Nafasi: Mshambuliaji

23.Mauro Icardi

Timu: Inter Milan

Nafasi: Mshambuliaji

24.N’Golo Kante

Timu: Chelsea

Nafasi: Kiungo mkabaji

25.Kalidou Koulibaly

Timu: Napoli
 
574a18ec-0e85-4b9d-982c-dc266201d776~2.jpg
 
Back
Top Bottom