Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

INGEKUWA uswahilini tungesema bakora zimekaribia Old Trafford. Lakini kwa Wazungu pale Manchester United mashabiki wamechukua njia nyingine ya kuonyesha kukerwa na utawala wa sasa wa Bosi Mtendaji, Ed Woodward.

Imebainika mashabiki wa United wameandaa ndege maalumu itakayobeba ujumbe wa kutomtaka bosi huyo katika pambano dhidi ya Burnley Septemba 2 utakaoandikwa ‘Ed Out’-LUHG’ (Love United, Hate Glazers).
 
Pambano hilo litapigwa ugenini katika Uwanja wa Turf Moor lakini mashabiki wa United wanataka kufikisha ujumbe wao kuonyesha jinsi ambavyo wanakerwa na masuala ya uhamisho wa wachezaji klabuni hapo.

Itakuwa mara ya kwanza kwa mashabiki wa United kuonyesha mabango hayo kwa njia hiyo tangu walipofanya hivyo kwa kocha wa zamani wa Manchester United, David Moyes ambaye alichemsha baada ya utawala wa Sir Alex Ferguson. Moyes alionyeshwa bango hilo Machi 2014 na alifukuzwa baada ya mwezi mmoja.
 
Woodward amekuwa na tofauti na Kocha Jose Mourinho kuhusu sera za uhamisho wa wachezaji klabuni hapo licha ya Mourinho kutumia Pauni 400 milioni kwa ajili ya wachezaji wapya katika kipindi cha miaka miwili alichokuwa klabuni hapo.

Cheche zimewaka zaidi baada ya beki wa zamani wa Manchester United, Gary Neville ambaye ni mchambuzi mahiri siku hizi England kudai Woodward alikuwa anamuhujumu Mourinho kwa kutompa pesa za kununua wachezaji licha ya kumpa mkataba mpya Januari.
 
Inaumiza kuona jinsi mambo yanavyofanyika katika kipindi cha miaka mitano au sita iliyopita. Kama Ed Woodward angekuwa na wasiwasi na Mourinho basi angefanya hivyo Januari iliyopita. Dakika ileile aliyompa mkataba mwingine Jose Mourinho ilibidi amnunulie mabeki wa kati,” alisema Neville.

“Ilibidi amnunulie (Harry) Maguire, ilibidi ampatie pia na (Toby) Alderweireld, kwa sababu wasingefanya makosa yaliyofanyika katika mechi ya Brighton. Mtazamo wangu Alderweireld na Maguire wangekuwa sahihi. Kama gharama ya kuwaleta ni Pauni 120 milioni basi hilo ndilo unaloweza kufanya kumsapoti Jose Mourinho.”
 
Ripoti nyingine za ndani zinadai mabosi wa United bado wanamsapoti kocha huyo wa zamani wa Chelsea lakini wana wasiwasi kuondoka kwa msaidizi wake wa muda mrefu, Rui Faria kunaweza kusababisha kocha huyo afeli klabuni hapo.

“Rui alikuwa ni mtu pekee ambaye alikuwa na uwezo wa kumdindishia Jose katika siku za nyuma na kumpa maneno ya maana yakamuingia. Walikuwa ni marafiki bora na usingewatenganisha. Hata hali ilivyo sasa ingeweza kuleta mzozo baina yao lakini Jose alimheshimu kuliko mtu mwingine yeyote,” alisema mtoa taarifa mmoja wa ndani.
 
“Sasa Rui ameondoka na hayupo kando yake, nani anajua kinachoweza kutokea? Nani anaweza kummudu Jose?”

Mourinho ameanza kupandwa na presha na kikosi cha United baada ya kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa vibonde Brighton wiki iliyopita. Amekuwa akikosolewa kwa mbinu zake za uwanjani pamoja na tabia za ajabu pia nje ya uwanja.
 
INGEKUWA uswahilini tungesema bakora zimekaribia Old Trafford. Lakini kwa Wazungu pale Manchester United mashabiki wamechukua njia nyingine ya kuonyesha kukerwa na utawala wa sasa wa Bosi Mtendaji, Ed Woodward.

Imebainika mashabiki wa United wameandaa ndege maalumu itakayobeba ujumbe wa kutomtaka bosi huyo katika pambano dhidi ya Burnley Septemba 2 utakaoandikwa ‘Ed Out’-LUHG’ (Love United, Hate Glazers).
Safi Sana Ed anazingua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]
tapatalk_1532351983809.jpeg
 
Back
Top Bottom