Safi Sana Ed anazinguaINGEKUWA uswahilini tungesema bakora zimekaribia Old Trafford. Lakini kwa Wazungu pale Manchester United mashabiki wamechukua njia nyingine ya kuonyesha kukerwa na utawala wa sasa wa Bosi Mtendaji, Ed Woodward.
Imebainika mashabiki wa United wameandaa ndege maalumu itakayobeba ujumbe wa kutomtaka bosi huyo katika pambano dhidi ya Burnley Septemba 2 utakaoandikwa ‘Ed Out’-LUHG’ (Love United, Hate Glazers).