Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Mshambuliaji Wayne Rooney amemwambia Paul Pogba kwamba suala la kuboresha kiwango chake ni lake binafsi sio la kocha Jose Mourinho.
Rooney amemwambia Pogba anapaswa kucheza kwa kiwango kikubwa anapoitumikia timu yake ya Manchester United kwani mafanikio yoyote yatakayopatikana kutokana na ubora wa uchezaji wake ndani ya uwanja, sifa zote zitaelekezwa kwake.
Kiungo huyo Mfaransa, Pogba alichaguliwa kuwa nahodha kwenye mechi zote mbili za kwanza ilizocheza kwenye ligi, lakini wikiendi iliyopita alicheza kwa kiwango cha hovyo sana wakati Man United ilipokumbana na kipigo cha kushtua kutoka kwa Brighton.
Kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018, Pogba alipewa sifa kubwa sana kutokana na kiwango chake cha soka ambacho kiliisaidia Ufaransa kunyakua ubingwa wa michuano hiyo. Lakini, huko Man United, kocha Mourinho amekuwa akishutumiwa kwamba hawezi kumtumia Pogba kwenye ubora wake, lakini Rooney anaamini kwamba hilo ni suala la mchezaji mwenyewe.