Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sijui kwann huwa sijali vitu kama hivi daah i wish niwe na hisia kama zako,ujue zile ligi naziendeshaga kiushabiki zaidi kuliko kihisia yaan kwangu ni kama naangalia epl,dakika 90 zikiisha naendelea na mambo mengine kama hakuna kilichotokea.
Kaisiki kange - kama haya unayosema ni kweli basi una elements za u-psychopath. Mtu wa kawaida lazima uwe na hisia bana [emoji16][emoji16][emoji16][emoji1549]‍♂️[emoji1549]‍♂️[emoji1549]‍♂️

Ukiua wadudu huwa una hisia zo zote? Wanyama je? Baes? [emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️[emoji1550]‍♂️
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mbio za nn sasa bagesh
 
Unaweza kushangaa kwa nini hupati kile unachokitafuta!Je unajua sababu ya kushindwa kutimiza ndoto zako ni wewe mwenyewe?
Utakubaliana na mimi kuwa sababu ya kushindwa kutimiza ndoto zako ni kwa sababu haujui nini unakitafuta na unakihitaji.

Watu wengi wamekuwa na hamu ya kupata mafanikio makubwa lakini wameshindwa kutofautisha hamu/shauku zao ambazo zimegawanyika katika viwango vitatu vya uhitaji.

Viwango hivi vitatu ambavyo vitakusaidia wewe kujua upo katika kiwango gani,pengine kupiga hatua kutoka katika kiwango ulichonacho kwenda kwenye kiwango kinachofuata
 
KIWANGO CHA "NINGEPENDA"
"Ningependa" neno hili huonyesha upenzi wa kitu fulani ambacho mtu anapenda kukipata au kuwa.Mfano Ningependa kuwa raisi,Ningependa kuwa tajiri.,,

Ningependa kuwa mfanya biashara mkubwa.Watu wengi wako katika kundi hili la kutaka kuwa mtu fulani lakini katika kundi hili hutumika nadharia tu, hakuna kitendo chochote kitakachotokea katika kiwango hiki cha kupenda.
 
KIWANGO CHA "KUTAKA"
Katika hatua hii watu husema nataka kuwa mtu fulanii ninataka kuwa mwandish mzuri,ninataka kuwa mwalimu mzuri.

Hatua hii inakusanya maandalizi madogomadogo pia ni hatua muhimu ya mwanzo inayokusanya vitendea kazi kwa ajili ya kuvitumia katika kusudio lako.

Kiwango hiki sio kiwango ambacho kinakuweka katika kilele cha mafanikio lakini ni kiwango cha pili cha muhimu cha maandalizi ya kukuweka kwenye kilele.
 
HATUA YA KUJITOA (KUFANYA KAZI)
Katika hatua hii ndipo watu huanza kufanya kile ambacho ndoto yao inataka iwe,bidii ndio funguo muhimu ambayo mtu anapaswa awe nayo katika kufanikisha jambo lake na kupiga hatua zaidi.Dhamira ndio kiini cha mambo yote kwa kunafanya kile ambacho umekidhamiria,kile ambacho kimekuwa ni ndoto yako ya kila siku.

Dhamiria kikamilifu katika ndoto zako,fanya kazi kwa bidii bila kuchoka,weka mipango na mikakati ya kuendeleza na kupanga ndoto zako hakika utakuwa umepiga hatua kubwa kimaendeleo na utaweza kufikia malengo yako na kupata kile unachkitafuta.
 
Ni tumaini langu kuwa haujambo rafiki yangu mpendwa na msomaji wa blog hii ya patamambo,leo katika makala haya ninakwenda kuangazia nguvu ya MAWAZO inavyoweza kubadilisha maisha yako hata ulimwengu.

Wazo ni nguvu ambayo imeleta mabadiliko makubwa katika dunia hii,uumbaji wa dunia na mali zote zilizopo ulianza na wazo.Mungu alimuumba Adamu baada ya kumuumba Adamu Mungu ALIWAZA Haipendezi mtu huyu kuishi peke yake ndipo alipompatia msaidizi wake ambaye kwa jina aliitwa Hawa.

Huu ni moja wa mfano ambao nimekupatia ndugu ili uelewe juu ya Nguvu ya Wazo ambavyo imekuwa tangu dunia kuumbwa.Wagunduzi wa sayansi na tekinolojia wote walianza na wazo kisha wazo hilo wakaliweka katika vitendo ndio maana leo tuna simu za mkononi,ndege,mitandao ya kijamii nk.
 
Je una wazo gani hapo ulipo,wazo lako lina nguvu,Wazo lako lina uwezo wa kukufikisha katika uhuru kifedha,Je wazo lako unaweza kuliweka katika uhalisia na kulifanyia kazi ili likuletee faida na kukupatia kipato?Haya ni maswali unayopaswa kujiuliza kabla ya kuliweka wazo lako katika vitendo.

Maisha yako yanaaksi mawazo yako uliyowaza mwaka uliopita,miezi iliyopita,juzi,jana na leo,maisha uliyonaho sasa umeyatengeneza kwa mawazo yako ya siku za nyuma kwa kujua au kutokujua,nguvu ya wazo lako ndio maisha ambayo unayoyaishi sasa na utaendelea kuyaishi kesho na kesho kutwa.
 
Sikiliza Rafiki nikuambie Kushindwa sio kitendo cha siku moja,huwezi kushindwa kwa usiku mmoja, kushindwa ni kosa ambalo unalifanya katika mawazo yako ni tabia ya kurudia rudia kosa kila siku hivyo matokeo yake sasa kosa hilo linakuletea matokeo hasi juu ya wazo lako.

Hivyo ulivyo ni zao la mawazo na tabia au matendo yako ambayo unayarudia rudia kuyafanya kila siku.Wewe ni maskini kwa sababu hauna tabia ya kuweka akiba kila mara,ni maskini kwa sababu mawazo yako hayaendani na vitendo vyako vya kila siku.
 
Kwaheri mwaka 2017 karibumwaka mpya wa 2018 hizi ni baadhi ya sauti za watu wengi ambao Mungu amewajaalia kuona mwaka Mpya.
Nianze kwa kukuambia kuwa Hongera sana rafiki kwa kuona mwaka 2018.

Kila mwanzo wa mwaka watu hupanga mipango mingi ili kuweza kusukuma maisha ya kila siku na kutimiza ndoto mbalimbalimbali.Ni vyema ndugu ukawa na mipango ambayo utaenda kuifanyia kazi mwaka huu 2018 na hakikisha kuwa mipango hiyo inafanikiwa kabla ya kumaliza mwaka 2018.

Rafiki unapoanza mwaka mpya kitu pekee kinachobadilika ni namba yaani 2017 - 2018 mambo mengine yote hubaki kama yalivyo,thamani ya pesa hubaki vilevile,masaa huhesabika vilevile,Dunia hulizunguka jua katika staili ileile,pumzi na hewa tunayovuta huwa ni ileile n.k.
 
Katika mwaka huu 2018 kitu pekee unachopaswa kubadili ni staili ya maisha uliyonayo unahitaji mabadiliko ya kifikra katika kufikia mafanikio yako, unahitaji mabadiliko ya kiroho ili kufikia malengo yako, unahitaji mabadiliko ya kimwili ili kuweza kufikia malengo yako,pia unahitaji kubadili mbinu za kuongeza thamani na faida katika biashara yako au kazi yako ili kweza kufikia malengo yako.

Unapoanza mwaka 2018 unakuwa na uhakika wa asilimia mia (100%) wa kufikia malengo yako,kadri siku zinavyokwenda ndivyo asilimia inavyozidi kupungua.

Mpaka kufikia tarehe 30/12/2018 wapo watakao kuwa wamepunguza asilimia zao za kufikia malengo na kufikia 80,70,10,20,95 hata wengine 98%.
 
Ningependa kila rafiki yangu katika mtandao huu anafikia malengo yake mwaka huu 2018 bila kujali ukubwa wa malengo hayo.

Fanya haya
1.Chukua Daftari andika malengo yako kumi unayofikiria kuyatimiza mwaka huu.
2. Chambua malengo yako Matano
3.Chambua tena malengo mengine matatu muhimu.
4. Andika lengo lako muhimu moja ambalo utaenda kulifanyia kazi kila kukicha.

Jikumbushe malengo yako muhimu matatu kila siku na ufanyie kazi lengo lako moja kila siku bila kusahau malengo yako mawili muhimu ambayo nayo utayafanyia kazimwaka huu 2018
 
Ningependa kila rafiki yangu katika mtandao huu anafikia malengo yake mwaka huu 2018 bila kujali ukubwa wa malengo hayo.

Fanya haya
1.Chukua Daftari andika malengo yako kumi unayofikiria kuyatimiza mwaka huu.
2. Chambua malengo yako Matano
3.Chambua tena malengo mengine matatu muhimu.
4. Andika lengo lako muhimu moja ambalo utaenda kulifanyia kazi kila kukicha.

Jikumbushe malengo yako muhimu matatu kila siku na ufanyie kazi lengo lako moja kila siku bila kusahau malengo yako mawili muhimu ambayo nayo utayafanyia kazimwaka huu 2018
 
Nukuu "Maisha ni magumu na hayajawahi kuwa rahisi" Dr. Makrita

Nimeanza nakuandika nukuu ambayo itaniongoza katika makala haya ambayo nimekuletea siku ya leo.Nukuu hii ni ya Mwalimu wangu wa masuala ya ujasiliamali na uwekezaji Dr. Amani Makrita.

Mwanadamu ameumbwa na lugha ya lawama hasa kipindi anaposhindwa kutekeleza malengo yake,tumesahau ya kuwa matatizo ya kijamii na kiuchumi yapo kila siku, katika mazingira ya sasa utasikia neno hili
 
Usawa huu wa Magufuli tutanyooka" Hizi ni sauti za watanzania wengi waliokosa tumaini la kesho na kujaribu kutoa lawama kwa Raisi aliye madarakani,ukitizama kwa mapana neno hilo linaashiria kuwa watu walitegemea kupewa pesa mikononi ama kupanga foleni kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa kwa ajili ya kupewa pesa,hata kama ingekuwa hivyo bado minong'ono juu ya hali ngumu ya maishi isingeisha.

Nadharia hii iko sahihi kwa asilimia 10 pia haiko sahihi kwa asilimia 90 ,serikali inatoa asilimia 10 tu kama mchango wake katika maendeleo ya kila mwananchi.Asilimia hizo kumi hutolewa kwa kupunguza bei za pembejeo na madawa,vitendea kazi,usalama wa raia na mali zake, kusimamia soko la ndani ili kusiwepo na mfumko wa bei n.k
 
Hizi asilimia 90 unapaswa kuzitafuta wewe,Mafanikio ya malengo yako, yapo mikononi mwako mwenyewe.Hebu fikiria Ndugu yangu, matajiri wa dunia wana mali kedekede lakini mpaka kesho wanaendelea kutafuta pesa bila kuchoka.

Yawezekana kabisa tukalalamika kuhusu ugumu wa maisha, lakini wimbo huu tusimhusihe kiongozi,taasisi wala kampuni fulani kuwa ndio sababu ya ugumu wa maisha huu ni wimbo ambao kila mwana mafanikio aukatae na kuukemea kwa nguvu zote, yawezekana sisi wenyewe tukawa sababu ya hali ngumu ya maisha kulingana na sababu ambazo nitaziorodhesha hapa.
 
UVIVU WA KUFIKIRI NA KUTENDA
Nikiwa natafakari jinsi ya kuianza siku ya siku ile, nilitizama pembezoni mwa ukuta wa nyumba na kuona majani ya tikiti yaliyotanda kuzunguka ua, lililokuwa karibu na chombo nachotumia kutupa taka kabla hazijaondolewa na Manispaa.

Nilitizama kwa makini Tikiti lile niligundua kuwa kwenye shina lake limebeba watoto watatu (matikiti) yenye ukubwa saizi ya ngumi.

Wazo jipya la biashara lilijengeka kichwani kwangu,nilikimbia mara moja mpaka katika duka la Pembejeo za Kilimo na kununua mbegu bora za matikiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…