Ushindi huo umeifanya Chelsea kushinda mechi zake zote tatu za Ligi Kuu msimu huu, lakini Kocha wake Maurizio Sarri ameshangazwa na namna Newcastle, walivyoamua kucheza kujilinda.
Alisema hajui ni kwa vipi kocha Rafa Benitez, aliamua kujilinda kuanzia mwanzo na kuwaachia Chelsea kuuchezea mpira kadiri walivyotaka.
Kocha huyo alisema alifahamu tangu mwanzo kuwa kutakuwa na ugumu kwenye mchezo huo ikizingatiwa Chelsea haijawahi kuondoka na pointi tatu, St James' Park, tangu Desemba, 2011, lakini katika mchezo wa jana ugumu uliongezeka.