Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mchezaji huyo mwenye miaka 31, aliibuka mshindi baada ya saa mbili akishinda kwa 6-7 (5-7) 6-3 7-5 6-3 alionekana kuhimili licha ya kucheza kwa muda mrefu hakuomba mapumziko.

Katika raundi ya pili ya mashindano hayo Murray mzaliwa wa Scotland atacheza na Fernando Verdasco kutoka Hispania, mjini New York.

Murray, ambaye ametwaa mataji matatu ya Grand Slam, amechukua muda mrefu kupona majeraha yake ya upasuaji wa goti aliofanyiwa kiasi cha kushindwa kutetea taji lake la Wimbledon mapema mwaka huu.
 
Alichokisema jana baada ya mechi kumalizika United wakiwa wamelowa kwa mabao 3-0 kutoka kwa wageni wao Tottenham Hotspurs, Kocha Jose Mourinho, aliwaambia waandishi neno moja tu, heshima, heshima heshima.

Baada ya kutamba neno hilo mara tatu, Mourinho alitoka kwenye ukumbi wa mikutano na kuondoka zake, ikionesha wazi kuwa anaugulia maumivu moyoni.

Hicho ni kipigo cha kwanza kikubwa kwa Mourinho sio tu tangu aanze kuinoa Manchester United lakini katika historia yake ya soka, kutokana na ukweli kwamba Kocha huyo amekuwa akisifika kwa staili yake ya kujilinda maarufu ‘kupaki basi’.
 
Baadaye katika kinachoonekana kama kujaribu kujifariji, Mourinho alisema yeye bado ni Kocha bora kwani ndiye aliyetwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu mara nyingi kuliko Kocha yeyote anayefundisha sasa katika Ligi hiyo.

“Mimi peke yangu nimetwaa ubingwa wa Ligi Kuu kuliko Makocha wengine wote 19 wanaozifundisha timu kwa msimu huu,” alitamba Mourinho.

Alisema kuwa katika mchezo huo walicheza mfumo wa kushambulia kwa nia ya kujipatia ushindi lakini mammbo hayakuwa vile walivyotaka, wakajikuta wakicheza vizuri na kumiliki mpira zaidi ya wapinzani wao.
 
Mabao kutoka kwa Harry Kane kwa kichwa dakika ya 50 na mawili kutoka kwa Lucas Moura dakika ya 52, 84 yaliwapa Spurs ushindi wa kwanza Old Trafford kwa zaidi ya muhongo mmoja.

Kabla ya mchezo wa jana, Tottenham Hotspur ilikuwa imecheza Old Trafford mara 26 tangu mwaka 1992 kushinda michezo miwili sare tatu na kupoteza michezo 21.

Ingawa Ligi Kuu England ndio kwanza imeanza lakini kwa matokeo haya kama United hawatashinda mechi tatu au nne zijazo, kibarua cha Mourinho kinaweza kuishia hapo.
 
UNAAMBIWA hivi, ukiwa na Pauni 2.5 bilioni tu, bilionea Roman Abramovich anakuuzia timu yake ya Chelsea.

Ripoti zinadai bilionea huyo wa Urusi anaweza kufikiria mpango wa kuuza Chelsea kama kutakuwa na ofa inayoanzia Pauni 2.5 bilioni, pesa ambayo wachambuzi wa mambo wamedai kimsingi hana mpango wa kuiuza klabu yake aliyoinunua mwaka 2003.

Imeelezwa Chelsea haina thamani hiyo, huku timu yenye thamani kubwa zaidi kama unataka kuinunua kwa sasa ujipange basi ni Manchester United, ambayo huwezi kuimiliki kama huna mkwanja unaoanzia Pauni 3.2 bilioni.
 
MAISHA ndivyo yalivyo. Unahitaji kuwa na pesa kufanya unachotaka kukifanya. Kawaulize Liverpool watakuthibitishia hilo.

Mwaka jana walitumia Pauni 34.3 milioni kunasa huduma ya Mohamed Salah kutoka AS Roma, akawafungia mabao 36 kwenye mechi 40 tu. Yalikuwa matumizi mazuri ya pesa, ambayo kimsingi ndiyo yaliyokuwa makubwa zaidi kutumika kwa mchezaji mmoja katika kikosi hicho chini ya Kocha Jurgen Klopp.

Mo Salah ameleta mambo matamu, Liverpool imefika hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kama si makosa ya kipa wake, basi mambo yangekuwa mengine kabisa katika fainali hiyo iliyocheza dhidi ya Real Madrid.
 
Kuona hivyo, kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi ya mwaka huu, Klopp ameamua kuingia zake sokoni na kutumia pesa nyingi tena kutafuta kile anachokitafuta. Akamnasa kipa Alisson Becker kutoka AS Roma kwa ada ya Pauni 67 milioni, kulifanya goli la timu hiyo kuwa salama tofauti na ilivyokuwa wakati wa Loris Karius.

Kumbuka kwenye dirisha la Januari, Klopp alitumia Pauni 75 milioni kupata huduma ya beki wa kati, Virgil van Dijk, kuja kucheza na Joel Matip, aliyembeba bure kabisa, Joe Gomez aliyenaswa kwa Pauni 3.5 milioni kutoka Charlton Athletic na Andrew Robertson aliyenaswa kwa Pauni 10 milioni kutoka Hull City.

Kisha Klopp akawanunua viungo wa kuwalinda mabeki wake hao, Naby Keita kwa Pauni 52.75 milioni kutoka RB Leipzig na Fabinho kutoka AS Monaco. Lakini, Mbrazili Fabinho bado hajaanza kutumika.
 
Klopp ameona pesa inalipa na mkwanja mrefu aliotumia kwenda kutengeneza safu yake ya ulinzi, umelipa pia. Kwenye Ligi Kuu England, kikosi hicho cha Anfield kimecheza mechi tatu, ugenini na nyumbani, lakini kwa mabeki waliotumika hadi sasa, hawajaruhusu bao lolote kwa dakika 270 walizocheza.
 
Klopp amewatumia mabeki wake wote na hakika wameonyesha mpira upo kwenye pesa kutokana na kikosi hicho cha Anfield kutoruhusu mpira wowote kwenye wavu wake huku washambuliaji wake kina Mo Salah na Sadio Mane wakitupia kwenye nyavu za wapinzani mara saba hadi sasa. Wakaki unasoma hapa, Liverpool ndio inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu England kwa kukusanya pointi tisa kwenye mechi tatu, mabao saba ya kufunga na haijafungwa bao lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…