Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mafua yanasababishwa na virusi vya aina mbalimbali. Kuna zaidi ya aina 200 ya virusi visababishavyo mafua. Kirusi aina ya ‘’rhinoviruses’’ ndicho kinachosababisha mafua kwa asilimia kubwa 30 hadi 80 ukilinganisha na virusi vya aina nyingine. Virusi vingine vya mafua ni human coronavirus, influenza viruses, adenoviruses, human parainfluenza viruses, human respiratory syncytial virus, enteroviruses, metapneumovirus n.k. Mara nyingi mtu anaweza kuambukizwa virusi vya mafua vya aina mbalimbali kwa maana ya kimoja au zaidi ya kimoja vyote katika kipindi kimoja.
 
VIPINDI AMBAVYO MAAMBUKIZI YA MAFUA YAPO JUU.

Kwa kawaida mlipuko wa mafua hutokea zaidi wakati wa mvua na baridi kali. Hii ni kutokana na uwezo wa virusi vya mafua kusambaa kwa kasi zaidi kipindi cha baridi kuliko vipindi vingine. Sababu nyingine ni kwamba wakati wa baridi ni rahisi kupata maambukizi ya virusi vya mafua kwa njia ya hewa kupitia mfumo wa kupumua.
 
SEHEMU AMBAZO NI RAHISI KUPATA MAAMBUKIZI YA MAFUA.

1. Utafiti umebaini kuwa watu wanaosafiri kwa ndege kwa muda mrefu kuanzia saa moja na kuendelea, wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa mafua.
Sababu hii kwa mujibu wa utafiti ni kwamba, kinga ya miili ya abiria wa kwenye ndege dhidi ya mafua huparaganyika kutokana na ukavu wa hewa ndani ya ndege. Unyevu wa hewa katika ndege inayosafiri zaidi ya saa moja hupungua kufikia kiasi cha asilimia 10 hadi 5.
 
Ukavu wa hewa au kupungua kwa unyevu katika hewa, husababisha vinywele (cilia) katika njia ya hewa kushindwa kukamata virusi vya mafua na kuvisafirisha hadi tumboni ambako kwa kawaida huunguzwa kwa tindikali (acid) ya tumboni na kufa. Mfumo wa upumuaji katika njia ya hewa huwa katika hali bora pale unyevu wa hewa unapokuwa kati ya asilimia 20 na 60.
 
Dalili zingine ni pamoja na kichwa kuuma, uchovu wa mwili, kupoteza hamu ya kula chakula na hali ya kuwasha kwa koo.
Dalili hizi huanza ndani ya saa 16 tokea wakati wa kugusana na virusi au visababishi vya mafua. Hali huwa mbaya katika kipindi cha saa 24 hadi 72 ambapo virusi huwa vingi katika majimaji yatokayo puani. Katika kipindi hiki mgonjwa wa mafua huwa na uwezo mkubwa wa kuambukiza watu wengine. Dalili za ugonjwa wa mafua hutegemea zaidi uwezo wa mwili kupambana na ugonjwa
 
Mafua yanaweza kusababisha matatizo makubwa katika mfumo wa kupumua hasa pale yanapoambatana na mambukizi ya pili mfano maambukizi mengine yaliyosababishwa na bakteria. Matatizo yanaweza kuwa makubwa zaidi kwa watoto wachanga, wazee au kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini.
 
NJIA ZA KUKABILIANA NA MAFUA.

Njia zinazosaidia kukabiliana na tatizo la mafua ni pamoja na

Kunawa mikono mara kwa mara na kuepuka kushika shika pua na macho.
Kufunika pua na mdomo kwa kitambaa wakati wa kupiga chafya.
Kupumzika muda wa kutosha.
Kunywa maji na juisi za matunda kwa wingi. Mfano juisi zilizotengenezwa na matunda yenye vitamin C kwa wingi kama mananasi, machungwa, malimao n.k
 
Kuondoa maumivu na homa ili kupata nafuu. Unaweza kuondoa maumivu kwa kumeza dawa za kutuliza maumivu. Mfano: Panadol, Paracetamol n.k
Kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.
Kula mboga mboga na matunda kwa wingi kwani ni njia bora ya kupunguza uwezekano wa kupata mafua mara kwa mara kwasababu vitamin C na madini ya zinc yanayopatikana katika vyakula hivi huongeza na kuimarisha kinga ya mwili.
 
Watu ambao Micheal aliwachagua kila mmoja alimteua kwa sababu maalumu kutokana na umuhimu fulani alionao ambao utahitajika katika kufanikisha tukio la kutoroka. Mfano alimchagua cell mate wake Fernando Sucre ili aje kuwasaidia katika mpango wa kuingia nchi ya Mexico kiurahisi baada ya kutoroka, alimchagua John Abruzzi ili aje kusaidia kupata usafiri wa ndege watokomee pindi tu wakitoroka Fox River, na wengineo wote waliojumuishwa kwenye mpango huo walikuwa na umuhimu maalum.
 
Swali je, fedha wanapata wapi? Ndipo hapo anapoingia Charles Westmoreland, ambaye licha ya kutumia jina hili la Charles Westmoreland, Michael Scofield aliamini kuwa huyu mzee ni D.B Cooper jambazi aliyefanikiwa kuiteka ndege na serikali kukubali kulipa dola milioni moja ili aiachie, jambazi ambaye mpaka mda huo alikuwa bado anatafutwa na FBI, jambazi pekee aliyefanikiwa kuweka historia katika nchi ya marekani kufanya tukio la utekaji ndege kwa mafanikio na kesi kushindwa kuwa kuwa solved na FBI kwa miaka 45! Licha ya Charles Westmoreland kukataa katakata kuwa yeye siye D.B Cooper lakini Michael aliamini yeye ndiye na fedha alizofanikiwa kulipwa na serikali bado hajazitumia ziko mahali fulani amezificha..
 
Baada ya majaribio kadhaa ya kumshawishi kushindikana, mwishoni kabisa Charles anakubali kuungana katika mpango wa kutoroka baada ya kugundua kuwa hatopewa fursa ya kumuona binti yake aliyekuwa anaumwa na ana karibia kufa, na kuthibitisha hilo anamuonyesha Michael noti ya fedha ya marekani yenye serial number D 1192589 ambayo ni moja ya noti katika fedha alizolipwa na serikali ili aweze kuiachia ndege aliyoiteka na baadae kabisa anakiri kwa Michael kuwa hakulipwa dola milioni moja kama inavyoripotiwa kwenye vyombo vya habari bali alilipwa dola milioni tano.
 
TUKIO LA KWELI KATIKA MAISHA HALISI.

Siku ya November 24 mwaka 1971, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mji wa Portland jamaa aliyevaa suti nyeusi na koti refu jeusi kwa juu akiwa amebeba brief case nyeusi alifika katika counter ya kampuni ya ndege ya Northwest Orient Airlines na akatoa fedha cash dola 20 kununua tiketi ya ndege Flight 305 kwenda mjini Seattle, ambayo kwa kawaida ni safari inayochukua dakika 30. Jamaa huyu alijitambulisha kama 'Dan Cooper'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…