Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tujadili hawa wachache;

1. Sir Isaac Newton.

(Mwanafizikia na mwanahesabu nguli)
Mtoto wa mkulima, tofauti na wengine Kidogo huyu alienda shule lakini alikuwa anasoma vitu vingine (philosophy)sio vile vilivyompa umaarufu. Upenzi wa hesabu aliupata alipojinunulia kitabu cha hesabu katika maonyesho. Newtons laws of motion, Formula nyingi za hesabu, uvumbuzi mwingi wa kisayansi tunaousoma kutoka kwa huyu jamaa alijifundisha na kubuni mwenyewe sio darasani. Leo watu wanakuwa maprofesor, wataalam kwa kusoma vitu hivi.
 
2. Malcom X.

Huyu alijifundisha mwenyewe Philosophy, sociology na Genetics. Akiwa gerezani aliweza kuikopi dictionary yote kwa muda wa miaka saba na kuwa bora kwa misamiati iliyomfanya awe mwandishi na mzungunzaji bora. Baadae alikuja kuwa mpiganiaji maarufu wa haki za binadamu na watu weusi.
 
3. Abraham Lincoln.

Rais wa marekani mwenye heshima ya hali ya juu na Genius aliyeongoza taifa hilo bila uzoefu wa kutosha wa uongozi. Akiwa mtoto akizuiwa na baba yake mambo ya shule,kuna kipindi alikuwa anasafiri umbali mrefu kwenda kuazima kitabu ili ajisomee hukohuko shambani. Bila huyu marekani leo ingekuwa vipande vipande, wazungu wengine walimchukia kwa kutetea watu weusi. Alitokea kijijini. Hakuwawh kwenda shule lakini alijifundisha mwenyewe sheria miaka mitatu. Huwezi kudefine neno Democracy bila kutoa kile alichokisema yeye.
 
4. ADOLF HITLER.

(Mwanasiasa)
Hakumaliza shule ya secondary kwa sababu ya uanaharakati. Alishindwa kujiunga chuo kusomea Ufundi sanifu kwa sababu hakuwa na vigezo (hakumaliza secondary). Baadae alitawal taifa la wasomi na kuisumbua dunia.
 
5. KARL MARX.

(Philosopher, economist, sociologist, journalist and
revolutionary socialist)
mjerumani mwenye asili ya uyahudi. Maisha yake mengi aliishi maktaba moja pale england akijisomea na kuandika concepts. Watu walikuja kumuelewa baada ya kifo chake. Leo sio tu watu tunajifunza aliyoandika, mchango wake uliigawa dunia katika itikadi mbili (ujamaa na ubepari).
 
6. Konstantin.
Tsiolkovsky

unapozungumzia Sayansi ya watu kwenda mwezini. Huyu mrusi ndio mbabe na moja ya waanzilishi. Aliacha shule kwa kuwa alikuwa hasikii vizuri na wazazi kufariki. Katika kujisomea akajikuta amependa physics na hesabu. Muda wake mwingi aliutumia maktaba kujisomea. Pamoja na kudhalaulika duniani ukweli ni kwamba maandiko yake zaidi ya 400 yalileta mapinduzi makubwa katika sayansi ya kurusha rocket ulaya na Marekani.
 
7. LEONARDO DA VINCI.

(Invention , painting, sculpting , architecture , science , music ,
mathematics, engineering, literature , anatomy, geology,
astronomy, botany , writing, history, and cartography )

Huyu ni kipaji maalumu, lakini vyote alijiendeleza mwenyewe. Alikuwa na uwezo wa kuchora mkono wa kushoto wakati huohuo mkono mwingine anaandika. Alikuwa anajua karibu kila kitu yaani super genius.
 
9. DAVID BEN GURION.

Huyu ndio baba wa taifa na muanzilishi wa israel ya sasa. Akiwa na umri wa miaka 18, aliachana na mambo ya shule akaanza kujisomea mwenyewe philosophy na kujifunza kigiliki kwa lugha asilia ili aweze kusoma vitu vingi katika uhalisia sio viivyotafsiriwa. Ndie aliyeanzisha mifumo yote ya israel ya sasa, ikiwepo vikosi hatari kabisa vya kijeshi. Alikuwa haamini uwepo wa Mungu.
 
10. NIKOLA TESLA.

Huwezi kuzungumzia mapinduzi ya sayansi bila kumtaja huyu mdau. Ana mkono wake katika karibu kila kitu cha technologia, vitu ambavyo walisema haviwezekani leo vinawezekana. Kwenye engine za ndege, telecom, IT, Magari, Rocket,Vifaa vya kijeshi, Umeme wa Maji etc. Aliamua kuacha shule na kutengeneza workshop yake na kuanza kuvumbua vitu lukuki. Vitu alivyokuwa anafanya alisababisha watu wamuite *mwanasayansi kichaa.* Ni baba wa AC ELectricity, alikufa akiwa na ndoto ya kutaka kuusafirisha umeme kwenye anga ili dunia nzima umeme uwe bure. Katika majaribio yeke aliwahi kusababisha tetemeko la ardhi mji mzima. Leo japan na marekani wanafanya research kama wanaweza kutransmit electrical signals from US to Japan kwa kutumia Anga
 
11. Mwanamama KATO LOMB.

Ni miongoni mwa watafsiri wa kwanza na pekee duniani mwenye uwezo wa kuafsiri lugha nyingi kwa mpigo (simultaneously Interpreter ). Alisoma degree ya CHemistry na Physics, baadae akagundua upenzi wake sio hiyo vitu ni Lugha. Akaamua kujifunza mwenyewe lugha zaidi ya 11 zilizomuingizia kipato kikubwa. Alijifunza kwa kujisomea vitabu au novel za lugha husika hadi anaielewa kwa kuforce.
Formula yake ya mafanikio Aliyoibuni ni *Invested time + Motivation = Inhibition.*

Aliweza kuongea na kutafsiri lugha zifuatao;
Bulgarian, Chinese, Danish, French, English, German, Italian, Hebrew, Polish, Latin, Romanian, Japanese, Spanish, Russian, Slovak, Ukrainian.
 
Back
Top Bottom