Kupitia chanjo hiyo, mamilioni ya watu na haswa watoto, ikiwemo mimi na wewe tumeweza kuuepuka ugonjwa huu, kwa chanjo za polio tulizopata tulipozaliwa⦠na hii yote ni kwa ajili ya jitihada za Jonas Salk, pamoja na timu yake ya watafiti.
Kitu nilichokipenda zaidi kwa Salk, ni kwamba: baada ya Chanjo hiyo kupatikana, angeweza kuiwekea hatimiliki, na kutajirika kwa mauzo yake, kama ambavyo makampuni mengi ya madawa yanafanya hivi sasaβ¦ Lakini, alipoulizwa kama angeiwekea hatimiliki chanjo hiyo, alijibu: βSiwezi kuiwekea hatimiliki, Je Waweza kuliwekea hatimiliki Jua? β