Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tatu simu zote kwenye chumba cha Mo Salah ziwe zimefungiwa, asipigiwe na mashabiki na asijumuishwe kwenye ishu zozote za kimatangazo, mahojiano au kwenda kusalimia wadhamini wa EFA kwa namna yoyote ile.

Nyingine ni katika mechi za kimataifa, Salah ni lazima asafirishwe na ndege kutoka hotelini hadi atakapohitajika kwenda.

Kusiwepo na mtu yeyote mwenye ushirika na EFA awe na uwezo wa kuomba kupiga picha au asainiwe chochote na staa huyo.
 
EFA imedaiwa wamekasirishwa na mahitaji hayo ya Mo Salah, lakini mwenyewe amesisitiza: “Haya mambo yamewekwa na kupuuzwa ili tu nionekane mpuuzi, mimi sio mpuuzi.

“Tumewatumia barua nyingi na mimi nipo hapa sitaki matatizo.”

Madai ya Mo Salah ni amekuwa hajioni kuwa huru anapokwenda kuichezea timu yake ya taifa kutokana na kumfanya kama sehemu ya dili mbalimbali za kibiashara zinazowanufaisha mabosi wa EFA.
 
Hata hivyo, kwa mujibu wa mwanasheria wake, staa huyo bado ana nia ya dhati ya kuendelea kuitumikia timu yake ya taifa.

Mo Salah kwa sasa amefunga mabao mawili kwenye Ligi Kuu England msimu huu ambapo kikosi chake cha Liverpool kinaongoza baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza, ikikusanya pointi tisa na mabao saba, huku ikiwa haijafungwa bao lolote.

Liverpool imepania kuweka historia ya Ligi Kuu England ikiwemo kutwaa ubingwa kuipoka Manchester City.
 
PEP Guardiola amewapiga mkwara makocha wenzake Jurgen Klopp na Maurizio Sarri wasichekelee yeye kupoteza pointi kwenye mechi dhidi ya Wolves kwa sababu ule utamu halisi wa Ligi Kuu England bado haujaanza.

Manchester City ilibanwa na Wolves na kutoka sare ya 1-1 wikiendi iliyopita, huku vikosi vya Liverpool na Chelsea vikishinda mechi zao na hivyo kuwa na rekodi nzuri ya kuanza msimu wa ushindi wa asilimia 100 baada ya kushinda mechi zote tatu za mwanzo wa msimu.

Hata hivyo, Kocha Guardiola amesema hakuna shida ya kuwa na wasiwasi wa jambo hilo kwa sababu ligi ndiyo kwanza ipo mwanzoni.
 
Man City waliweka rekodi kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita, ikibeba ubingwa kwa pointi kibao na Guardiola amebainisha mpango wake ni kurudia rekodi hiyo. “Baada ya mechi moja, ambayo tutacheza na Newcastle United yatakuja mapumziko ya mechi za kimataifa,” alisema Pep.

Baada ya hapo, tukirudi ndio ligi inakuwa inaanza rasmi, kwa sababu kutakuwa mechi moja baada ya nyingine, mambo mfululizo. Tunafahamu ugumu utakavyokuwa, lakini kwa wakati huo tutakuwa tumeshafanya maandalizi mazuri ya kuikabili Newcastle ambayo imekuwa na safu nzuri ya ukuta.” Man City itakwenda kumenyana na Liverpool Anfield, Oktoba 7 na hapo ndiyo taswira halisi ya mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England itakapojionyesha bayana.
 
KINACHOELEZWA, kiungo Paul Pogba amewasilisha maombi ya kuihama Manchester United kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya ili kutimkia kwenye timu nyingine.

Kwa mujibu wa gazeti maarufu la michezo huko Hispania, Marca Pogba ametoa mapendekezo hayo baada ya kuona Barcelona ipo tayari kuinasa huduma yake, lakini shida ni mabosi wa Man United hawapo tayari kumwaacha aondoke.
 
Wakala wa staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa, Mino Raiola, amekuwa akifanya kazi kubwa kuhakikisha mteja wake anaondoka Old Trafford kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi ili kuachana na wababe hao wa England, lakini shida Man United haipo tayari kufanya biashara hiyo.

Barca imepanga kuivamia Man United kwenye siku ya mwisho ya usajili na mkwanja wa Euro 100 milioni ili kumnasa staa huyo aliyetokea kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Les Bleus huko Russia mwezi uliopita.
 
STAA wa zamani wa Brazil, Ronaldo De Lima ameripotiwa yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha kuinunua klabu ya Real Valladolid inayoshiriki Ligi ya La Liga.

Valladolid ina deni linalokadiriwa kuwa ni Pauni 19.3 milioni, hivyo jambo hilo linamfanya rais wake, Carlos Suarez kushawishika kuiuza klabu hiyo kwa straika wa zamani wa Real Madrid, Ronaldo, ambaye amekuwa na hisa kwenye klabu ya Fort Lauderdale Strikers na sasa Cadena Ser inaripotiwa anakaribia kuwa mmiliki wa Valladolid.

Hata hivyo, Ronaldo anakabiliwa na upinzani mkali kwa sababu kuna mabosi wengine ambao wapo tayari kulipia kiasi hicho cha pesa anachotaka Suarez kwa ajili ya kunasa umiliki wa klabu hiyo.
 
USUPASTAA gharama sana, asikwambie mtu. Ukitaka kulifahamu hilo, basi waulize maofisa wa Chama cha Soka cha Misri baada ya kuambiwa na Mohamed Salah wajiuzulu wote, la sivyo basi wahakikishe mchezaji huyo hasumbuliwi anapokwenda kwenye mechi za kimataifa.

Staa huyo wa Liverpool amedai mashabiki wa Misri walikuwa wakimsumbua sana, wakijazana hotelini kwake na kumgongea mlango nyakati za usiku kisha wanataka tu asaini vitabu na jezi zao au kupiga picha na mchezaji huyo jambo ambalo mwenyew amelitafsiri kuwa ni kero kwake.
duh!!
 
FB_IMG_1535521602303.jpg
 
*HEPATITIS*

Hepatitis (Homa ya Ini) ni maambukizi ya virusi kwenye Ini(Liver) .
Ini likiambukizwa hatuna matibabu kamili na yakueleweka Tanzania.
Hepatitis (Homa ya Ini) imekuwa tishio kwa miaka hii na hasa kwa vijana.

*JINSI HOMA YA INI INAVYOENEA*

1.Ngono isiyo salama

2.Kuchangia nguo(Jasho na maji maji)

3.Romance(maji maji)

4.Kuchangia vifaa vyenye ncha kali.

*DALILI ZAKE NI ZIPI*?

Dalili zake hutokea wakati wa hatua za mwisho za kuharibika kwa Ini. kwa hiyo hakuna dalili za awali za ugonjwa huu.

01. Macho na mwili kuwa na rangi ya njano.

02.Tumbo kuvimba

03.Kutapika damu

04.Kukosa hamu ya kula kabisa.

05.Tumbo kuvimba(Abdominal distention)

6.Tumbo kuuma linapokugwa hasa sehemu ya ini(Epigastric pain on palpation)

*MATIBU YAKE YAKOJE*

Bado ni changamoto na hasa kwa Tanzania kwani ni wachache sana wanaopenda kupima afya na kujua hali zao za Ini na hivyo kuchukua hatua .
Kwa kuwa dalili hujitokeza dakika za mwisho za kufa kabisa kwa Ini kwa hiyo tiba kamili ni kubadilisha Ini kitu ambacho mazingira yetu ni changamoto sana.

Note:Ini liko moja tu tofauti na figo ambayo yako mawili kwahiyo hata kubadilisha ina mhitaji mtoaji afe ili mgonjwa aishi.

*CHANJO YA HOMA YA INI*

Siyo wote wanaweza kupata ugonjwa huu,ukipata chanjo uko salama kwa asilimia 100%

*NANI YUKO HATARI KUPATA UGONJWA HUU*

01.Wanaofanya ngono uzembe na hali hawana chanjo.

02.Wafanyakazi wa Idara ya afya hasa wauguzi na madaktari wanaogusa wagonjwa mara kwa mara bila kutumia chanjo!

03. Watoto wanaozaliwa na mama mwenye vimelea vya virusi vya homa ya Ini.

*MABARAZA YA DUNIA YANASEMAJE KUHUSU UGONJWA HUU*

01.Kila mjamzito anaye anza kliniki kwa mara ya anatakiwa kwanza lazima apime ugonjwa huu ili kumlinda mtoto anayezaliwa.
Kwa Bahati mbaya wanao pimwa ni wale wenye uwezo na wenye bima za afya ambao hujifungulia kwenye hospitali kubwa na zenye vifaa;
Mfano:- Agakhan, TMJ,KAIRUKI,Hindu mandal,Mbeya rufaa,Bugando,Selian,n.k

Note:Kiwango cha vifo vya vijana wa kiume kwa ugonjwa huu ni kubwa sana ukilinganisha na wanawake.

*UFANANO NA UTOFAUTI WA HOMA YA INI NA UKIMWI*

A.UFANANO

Hepatitis ina fanana na ugonjwa wa ukimwi kwa muktadha huu,

1.Jinsi Ukimwi unavyo enea ni sawa na Hepatitis

2.Hakuna tiba rasmi kwa magonjwa haya yote mawili.

B) UTOFAUTI

1.Homa ya Ini inachanjo,Ukimwi hauna

2.Ukimwi una dawa za kurefusha maisha,Hepatitis haina unapewa dawa za kupunguza maumivu ukisubiri kuondoka!

3.Virusi vya Homa ya Ini hukaa kwenye maji maji ,Mate(Denda) ,Jasho na damu. Wakati virusi vya Ukimwi hukaa kwenye damu tu.

4.Virusi vya homa ya Ini hukaa nje ya mwili(Kwenye nguo,wembe n.k) kwa siku saba,wakati virusi vya ukimwi hukaa dakika 30 tu.

5.Ugonjwa wa Ini ukiona dalili zake baada ya miezi sita mgonjwa hufariki, Wakati ukimwi ukiona dalili na ukiwahi hospitali una ishi miaka zaidi na zaidi.
******************************





Asante sana kwa taarifa na elimu pia kuhusu ugonjwa huo mbaya
 
MOTO unawaka huko Old Trafford. Kila mtu sasa anazungumza lugha yake. Wachezaji wanasema lao, bosi Ed Woodward anasema lake na Kocha Jose Mourinho, naye anasema lake.

Kocha Mourinho baada ya kikosi chake kupigwa 3-0 na Tottenham Hotspur, ameibuka na kauli ya kuwashangaza wengi, akidai yeye ndiye kocha bora zaidi kwenye Ligi Kuu England kwa sababu ana mataji matatu ya Ligi Kuu England, hakuna mwingine kwenye timu 19 nyingine zilizopo kwenye ligi hiyo mwenye idadi kama hiyo ya mataji.

Hata hivyo, wachezaji wake wameshakuwa na hofu kubwa, wanaamini kama kocha wao amebakiza mechi moja tu kufutwa kazi huko Old Trafford.

Kocha mwenyewe ana kiburi, anajiona na kujisikia, acha yamkute tu
 
USUPASTAA gharama sana, asikwambie mtu. Ukitaka kulifahamu hilo, basi waulize maofisa wa Chama cha Soka cha Misri baada ya kuambiwa na Mohamed Salah wajiuzulu wote, la sivyo basi wahakikishe mchezaji huyo hasumbuliwi anapokwenda kwenye mechi za kimataifa.

Staa huyo wa Liverpool amedai mashabiki wa Misri walikuwa wakimsumbua sana, wakijazana hotelini kwake na kumgongea mlango nyakati za usiku kisha wanataka tu asaini vitabu na jezi zao au kupiga picha na mchezaji huyo jambo ambalo mwenyew amelitafsiri kuwa ni kero kwake.

Asee
 
Back
Top Bottom