Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tatu simu zote kwenye chumba cha Mo Salah ziwe zimefungiwa, asipigiwe na mashabiki na asijumuishwe kwenye ishu zozote za kimatangazo, mahojiano au kwenda kusalimia wadhamini wa EFA kwa namna yoyote ile.

Nyingine ni katika mechi za kimataifa, Salah ni lazima asafirishwe na ndege kutoka hotelini hadi atakapohitajika kwenda.

Kusiwepo na mtu yeyote mwenye ushirika na EFA awe na uwezo wa kuomba kupiga picha au asainiwe chochote na staa huyo.
 
EFA imedaiwa wamekasirishwa na mahitaji hayo ya Mo Salah, lakini mwenyewe amesisitiza: “Haya mambo yamewekwa na kupuuzwa ili tu nionekane mpuuzi, mimi sio mpuuzi.

“Tumewatumia barua nyingi na mimi nipo hapa sitaki matatizo.”

Madai ya Mo Salah ni amekuwa hajioni kuwa huru anapokwenda kuichezea timu yake ya taifa kutokana na kumfanya kama sehemu ya dili mbalimbali za kibiashara zinazowanufaisha mabosi wa EFA.
 
Hata hivyo, kwa mujibu wa mwanasheria wake, staa huyo bado ana nia ya dhati ya kuendelea kuitumikia timu yake ya taifa.

Mo Salah kwa sasa amefunga mabao mawili kwenye Ligi Kuu England msimu huu ambapo kikosi chake cha Liverpool kinaongoza baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza, ikikusanya pointi tisa na mabao saba, huku ikiwa haijafungwa bao lolote.

Liverpool imepania kuweka historia ya Ligi Kuu England ikiwemo kutwaa ubingwa kuipoka Manchester City.
 
PEP Guardiola amewapiga mkwara makocha wenzake Jurgen Klopp na Maurizio Sarri wasichekelee yeye kupoteza pointi kwenye mechi dhidi ya Wolves kwa sababu ule utamu halisi wa Ligi Kuu England bado haujaanza.

Manchester City ilibanwa na Wolves na kutoka sare ya 1-1 wikiendi iliyopita, huku vikosi vya Liverpool na Chelsea vikishinda mechi zao na hivyo kuwa na rekodi nzuri ya kuanza msimu wa ushindi wa asilimia 100 baada ya kushinda mechi zote tatu za mwanzo wa msimu.

Hata hivyo, Kocha Guardiola amesema hakuna shida ya kuwa na wasiwasi wa jambo hilo kwa sababu ligi ndiyo kwanza ipo mwanzoni.
 
Man City waliweka rekodi kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita, ikibeba ubingwa kwa pointi kibao na Guardiola amebainisha mpango wake ni kurudia rekodi hiyo. “Baada ya mechi moja, ambayo tutacheza na Newcastle United yatakuja mapumziko ya mechi za kimataifa,” alisema Pep.

Baada ya hapo, tukirudi ndio ligi inakuwa inaanza rasmi, kwa sababu kutakuwa mechi moja baada ya nyingine, mambo mfululizo. Tunafahamu ugumu utakavyokuwa, lakini kwa wakati huo tutakuwa tumeshafanya maandalizi mazuri ya kuikabili Newcastle ambayo imekuwa na safu nzuri ya ukuta.” Man City itakwenda kumenyana na Liverpool Anfield, Oktoba 7 na hapo ndiyo taswira halisi ya mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England itakapojionyesha bayana.
 
KINACHOELEZWA, kiungo Paul Pogba amewasilisha maombi ya kuihama Manchester United kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya ili kutimkia kwenye timu nyingine.

Kwa mujibu wa gazeti maarufu la michezo huko Hispania, Marca Pogba ametoa mapendekezo hayo baada ya kuona Barcelona ipo tayari kuinasa huduma yake, lakini shida ni mabosi wa Man United hawapo tayari kumwaacha aondoke.
 
Wakala wa staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa, Mino Raiola, amekuwa akifanya kazi kubwa kuhakikisha mteja wake anaondoka Old Trafford kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi ili kuachana na wababe hao wa England, lakini shida Man United haipo tayari kufanya biashara hiyo.

Barca imepanga kuivamia Man United kwenye siku ya mwisho ya usajili na mkwanja wa Euro 100 milioni ili kumnasa staa huyo aliyetokea kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Les Bleus huko Russia mwezi uliopita.
 
STAA wa zamani wa Brazil, Ronaldo De Lima ameripotiwa yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha kuinunua klabu ya Real Valladolid inayoshiriki Ligi ya La Liga.

Valladolid ina deni linalokadiriwa kuwa ni Pauni 19.3 milioni, hivyo jambo hilo linamfanya rais wake, Carlos Suarez kushawishika kuiuza klabu hiyo kwa straika wa zamani wa Real Madrid, Ronaldo, ambaye amekuwa na hisa kwenye klabu ya Fort Lauderdale Strikers na sasa Cadena Ser inaripotiwa anakaribia kuwa mmiliki wa Valladolid.

Hata hivyo, Ronaldo anakabiliwa na upinzani mkali kwa sababu kuna mabosi wengine ambao wapo tayari kulipia kiasi hicho cha pesa anachotaka Suarez kwa ajili ya kunasa umiliki wa klabu hiyo.
 
duh!!
 
 

Kocha mwenyewe ana kiburi, anajiona na kujisikia, acha yamkute tu
 

Asee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…