Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Katoka kazini, kashuka kwenye basi anakwenda home, ghafla majambazi na mapanga wakamkatakata!
Professor alikuwa simple sana, na brilliant walahi!
Yaani ile miakili yote jamani uwiii!
Asante sis. Najua umejitahidi sana kuandika yote haya kwa sababu siyo kawaida yako.

Karma will get them. Hawatabaki salama - wao na vizazi vyao. Kama ni kumpora mbona wasingechukua wanavyotaka na kwenda zao? Au walikuwa wametumwa kummaliza profesa wa watu?

Maprofesa hawa mabingwa tunao wachache sana na kuwasomesha ni kazi kweli kweli. Hata tulionao sidhani hata kama tunawaangalia vizuri na kuwajali. Inahuzunisha sana. Pumzika salama prof. Umetangulia tu na waliokutanguliza nao watakuja huko huko kujibu...
 
MCHAPO(WHISK): Hii ni aina ya mashine ya kuchanganya unga ukitumia mkono (sio ya umeme) muhimu kuchanganya mayai au unga lakini inachukua mda mwingi. Unaweza kuanzia kupika keki kwa kuchangannya mahitaji yako ukitumia mchapo, lakini kama unataka kupika keki za biashara utahitaji mashine za umeme kukurahisishia kazi!
 
MASHINE ZA KUCHANGANYA UNGA (ZA UMEME)/ELECTRIC MIXERs; Kama unataka kupika keki za biashara, nakuhusia upate mashine ya kuchanganya unga ya umeme kwani inarahisisha kazi sana na keki haikupigi chenga! Sio lazima kuwa nayo lakini kuwa nayo ni kama umeajiri mikono miwili zaidi jikoni! huku mashine inakufanyia kazi ww unafanya kazi nyengine!
Ziko aina nyingi na kila brand za mashine ina kazi yake kulingana na ukubwa, nguvu yake nk, Kwa hivyo kabla hujanunua mashine, jiulize unataka kuitumia kwa kazi gani, utaitumia mda gani, inachanganya unga kilo ngapi kwa mara moja, nk
 
5 MIIKO SPESHELI YA KEKI (SPATULAS): Miiko hii nayo pia inapatikana ya chuma au plastiki, na ukubwa tofauti pia. Hii muhimu kwa kutoa/kufuta mchanganyiko wote kwenye beseni kutia kwenye kibati cha kuoka nk. (sio utumie mikono au vidole vyako!!!) Pia inatumiwa kusawazisha juu ya keki kabla kuokwa.
Miiko hii muhimu pia utatumia kwenye kupambia keki.

YA CHUMA (inaitwa); pallete knife, angle knife
YA PLASTIKI (inaitwa) Spatula
 
OVEN/MOTO WA KUOKEA KEKI: Oven nalo muhimu kwa mapishi ya keki hasa kama unataka kuunda keki za biashara. Lakini nasisitiza sio lazima!. Kama huna oven, unaweza kupambia keki kwenye sufuria kutumia mkaa/makaa. Lakini kwa urahisi wa mapishi oven ni muhimu. Ikiwa huna unaweza kuanza biashara yako ukitumia moto wa mkaa/makaa lakini ujipange ununue oven la biashara ukifanikiwa kiuchumi.
Kumbuka nayo ma oven pia yapo tofauti tofauti. Muhimu ambayo yapo kwa wingi ni:
 
CONVECTIONAL OVENS (pia zinaitwa THERMAL au RADIANT OVEN):
oven hizi zinakuwa na wire ambazo utaziona zimeshika moto sehemu ya juu (zikiwa moto zinakuwa nyekundu) Oven hizi zinapika chakula kwa kusukuma upepo wa baridi kuelekea chini ya oven pindi sehemu ya juu inakuwa moto. Kwa hivyo huo upepo unaoshuka chini unaweza kufanya keki yako isiive uzuri au ikupige chenga,
Kama unalo oven, liangalie ndani ujue una oven aina gani ndio ulifahamu oven lako!
 
CONVENTION OVEN: Oven hizi zinakuwa na kifaa cha kupuliza upepo (fan)(ambacho kawaida kinakuwa ndani lakini nyuma mwa oven lako). Upepo wa joto unapulizwa mwote ndani ya oven kwa hivyo keki inaiva haraka na kwa uzuri sana. Kwa ajili hiyo, mda wa mapishi kawaida unakuwa mfupi kulinganisha na oven lilotajwa hapo juu la convectional oven.

KWA HIVYO LITAMBUE OVEN LAKO!! Unaweza kupika keki ukafuata maagizo yote lakini ukaona imeungua kwenye kuokwa japo umeoka kwa mda ulopewa wa recipe. Basi ujue labda oven unalotumia ni 'convection oven' kwa hivyo mda ulifaa uupunguze kidogo! Nadhani hapo umeelewa? Lifahamu oven lako!

ANGAZO: Kumbuka hata maoven ya brand moja pia yanatofautiana, muhimu ni ulijue oven lako binafsi kwa kulifanyia mazoezi mpaka uliewe ndio utajua wapi unakosea kwenye upishi wa keki.
 
Back
Top Bottom