Jana nilikwenda katika mashine ya ATM kuchukua fedha. Nilikuwa na uhitaji mkubwa sana wa fedha kwa wakati huo.
Nilipofika tu, mashine ilinikaribisha kwa kuniambia niingize kadi yangu (Please insert your card.)
Nikafanya hivyo.
Baada ya kuingiza tu, ikaja meseji iliyonitaka niingize Nywila (password).
Nikafanya hivyo.
Kisha, meseji nyingine tena ikaja ikiniambia niingize kiasi nachotaka kuchukua
Nikafanya hivyo.
Baada ya kumaliza yote, Mashine ya ATM ikanionesha meseji yenye maandishi makubwa.
"MUAMALA WAKO UNAFANYIWA KAZI, TAFADHALI SUBIRI" (YOUR TRANSACTION IS BEING PROCESSED, PLEASE WAIT).
Nikawa nasubiri kwa muda mrefu mno bila fedha zangu kutoka!
Basi, kutokana na hayo, niruhusu nikwambie hili, endapo umefanya kila kitu kwa uwezo wako, umesali, umefunga, umewaomba hata wengine wakuombee lakini hakuna mabadiliko yoyote katika maisha yako, nakusihi usikate tamaa, kwa sababu maombi yako bado yanafanyiwa kazi na muda wowote utajibiwa.
SUBIRI!!
Ngoja tena nikwambie na hili. Kilichonifanya nisubiri kwa muda mrefu muamala ukamilike ni kwa sababu kadi yangu ya benki ilikuwa tayari ndani ya mashine na nilikuwa nimeshaingiza password.
Kama ningekata tamaa, nikajitoa ufahamu na kuondoka, mtu mwingine angekuja na kuchukua kiasi cha pesa nilichokuwa nimeomba kukichukua.
Hivyo, sio kwamba ujumbe wako kwa MUNGU haufiki, sio kwamba maombi yako sio sahihi, sio kwa sababu kufunga kwako ni bure..bali ni kwamba;
MUAMALA WAKO UNAFANYIWA KAZI!
Endelea kusubiri, usikate tamaa. Maana, kwa kufanya hivyo utamkaribisha shetani akuendeshe anavyotaka na kwa hakika utakula hasara mara elfu. Usifikiri ulizaliwa ili uhangaike. Maombi yako yanafanyiwa kazi [emoji120]
Najua sio rahisi kukutia moyo, ila amini katika kusubiri. Maana, wakati wa MUNGU ni bora kuliko wakati mwingine wowote ule.
"Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu, watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mabawa kama tai; watakimbia bila kuchoka; watatembea bila kulegea." - ISAYA 40:31
MUAMALA WAKO UNAFANYIWA KAZI. TAFADHALI SUBIRI!
Mwenyezi MUNGU akubariki sana!.
Sent using
Jamii Forums mobile app