Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameshusha pumzi baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini kwenye mchezo wa Ligi Kuu England leo Jumapili.

Ushindi huo ni faraja kwa Mourinho baada ya kuwapo kwenye presha kubwa ya kupoteza mchezo uliopita kutokana na kuchapwa mabao 3-0 dhidi ya Tottenham wiki iliyopita.

Mabao ya United yaliwekwa wavuni na Romelu Lukaku dakika ya 27' na 44'.

Nyota wa timu hiyo Marcus Rashford alikumbana na adhabu ya kadi nyekundu dakikaya 71 muda mfupi baada ya kuingia akichukua nafasi ya Alexis Sanchez.
 
Timu ya Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 kwenye uwanja wa ugenini na kuwafanya mashabiki wa klabu hiyo kuondoka na tabasamu zito uwanjani hapo.

Uamuzi wa Kocha wa Arsenal, Unai Emery kuwachezesha Pierre Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette tangu mwanzo wa mchezo imekuwa msaada wa timu hiyo na kuwafanya kuibuka na ushindi huo mnono.

Hadi timu hizo zinakenda mapumziko mabao yalikuwa 1-1 ambapo bao la Arsenal lilifungwa na Shkoran Mustafi dakika ya 11' huku bao la kusawazisha la Cardiff likiwekwa wavuni na Victor Camarasa dakika ya 45'.

Aubemameyang aliweka wavuni bao la pili dakika ya 62' huku Danny Ward akiisawazishia timu yake bao dakikaya 70'.

Msumari wa mwisho na bao la ushindi liliwekwa wavuni na Lacazette dakika ya 81' huku Harry Arter wa Cardiff akiambulia kadi ya njano dakika ya 90'.
 
. Jinamizi la mshambuliaji nyota wa Juventus Kibibi Kizee cha Turin Cristiano Ronaldo, linaendelea kumuandama katika Ligi Kuu Italia.

Mshambuliaji huyo ameshindwa kufunga bao katika mechi tatu alizocheza Juventus ikiwemo ya juzi usiku walioshinda mabao 2-1 dhidi ya Parma.

Ronaldo aliyekuwa kinara wa kufunga mabao Real Madrid kabla ya kutua Juventus majira ya kiangazi, alipewa matumaini ya kufungua ukarasa mpya katika mchezo huo.

Licha ya kuonyesha kiwango bora, lakini Ronaldo hakufurukuta mbele ya mabeki wa Juventus.

Mabao ya Juventus katika mchezo huo yalifungwa na mshambuliaji nguli Mario Mandzukic na Blaise Matuidi.

Bao la Parma katika mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Gervinho.

Licha ya Juventus kuendelea kupata ushindi katika mechi tatu, Ronaldo ameshindwa kufua dau na kuanza kuibua maswali kwa mashabiki wa soka Italia
 
Alexis Sanchez amejiengua katika kikosi cha Chile kwa mechi mbili za kirafiki dhidi ya Japan na Korea Kusini.

Sanchez ametoa sababu za kujiengua ni kutaka kujikita katika kikosi cha Manchester United.

Uamuzi wa mchezaji huyo nyota wa zamani wa Barcelona na Arsenal umepokewa kwa furaha na kocha wa Man United Jose Mourinho.

Mourinho alisema ni jambo la kufurahisha mshambuliaji huyo mwenye miaka 29 kuona thamani ya klabu hiyo inayopambana kurejesha ubora wake.

Sanchez amekuwa na hali ngumu tangu alipojiunga na klabu hiyo baada ya kufunga mabao matatu katika mechi 20 alizocheza.

Mshambuliaji huyo aliwaambia viongozi wa Chama cha Soka Chile, hatakwenda Japan na Korea Kusini wiki ijayo kwa kuwa anataka kuisaidia Man United katika mechi za Ligi Kuu.

Alisema kitendo cha Man United kuanza vibaya msimu huu kwenye ligi kimempa presha mchezaji huyo anayepambana kupata namba katika kikosi cha kwanza.

“Hatajiunga na timu ya Taifa kwa mechi mbili dhidi ya Japan na Korea Kusini, ni uamuzi mzuri kwa sababu tunakabiliwa na mchezo ujao na Watford kabla ya kucheza mechi ya kimataifa,” alisema Mourinho.
 
Kocha Julen Lopetegui amesifu kiwango cha mchezaji wake katika kikosi cha Real Madrid Karim Benzema.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, amefunga mabao manne katika mechi mbili alizocheza kwenye mashindano ya Ligi Kuu Hispania msimu huu.

Lopetegui ametoa kauli hiyo baada ya Real Madrid kupata ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Leganes ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Mabao ya nahodha Sergio Ramos, Gareth Bale na Benzema, alimpa raha kocha huyo aliyejaza nafasi ya Zinedine Zidane.
 
Back
Top Bottom