Kocha wa Manchester City Pep Guardiola, ametoa maelekezo mapya kwa wachezaji wake akisema hataki soka ya kuremba katika Ligi Kuu England.
Guardiola amesema anataka kushinda kila mchezo lengo ni kutetea ubingwa wa mashindano msimu huu.
Kocha huyo alitoa kauli hiyo muda mfupi, baada ya Man City kuvuna pointi tatu kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United kwenye Uwanja wa Etihad.
Alisema jambo la kwanza ni kushinda mechi sio kucheza soka ya kufurahisha mashabiki isiyokuwa na faida kwa timu.
“Sitaki mpira wa kuremba, nataka ushindi kwa sababu naipenda kazi yangu. Ni rahisi ukiniangalia usoni kubaini nahitaji nini nikiwa uwanjani,” alisema Guardiola.