Toure amerejea kwenye kikosi hicho chenye maskani yake huko Athens, ambako alicheza kwenye msimu wa 2005-06, wakati ambapo alifunga mabao matatu katika mechi 20.
"Ni heshima kubwa sana kurudi Olympiacos! Nilipoondoka hapa mwaka 2006 nilisema kwamba siku moja nitarudi na nimefurahi kutimiza ahadi yangu," alisema Toure.
"Nilipata ofa kibao kutoka klabu nyingi za Ulaya, Asia na Marekani. Lakini, nifanya uamuzi wangu kutokana na uhusiano mzuri uliopo baina yangu na klabu hii. Bado nina njaa ileile ya mafanikio kama nilivyokuja hapa wakati ule, twende kazi!"