Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

a6b4a53b-e1de-4fee-920d-df785563472a.jpg
 
WAZAZI tunajua Darasa la SABA wataanza MTIHANI WA TAIFA Kesho tarehe 05-09-2018, Mungu awabariki wafanye vizuri. Mambo muhimu ya kuzingatia:

1. Muda umekaribia na watoto wamesoma vizuri waambieni waamini watafaulu na kesho waingie kwenye mtihani bila wasiwasi.

2. Mzazi Jali sana afya ya mtoto wakati huu. Asichelewe kulala, Ale chakula na kunywa maji safi na salama na atumie neti ya mbu wakati wa kulala. Mombee Mungu kila siku naye ataendelea kumpa afya njema.

3. Siku ya mtihani ikifika: Andaa vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya mtihani, kisha afike mapema kwenye chumba cha mtihani angalau nusu saa kabla ya mtihani. Mfundishe aombe Mungu angalau hata kwa dakika moja kisha awe na imani Mungu atamsaidia. Baada ya hayo atulize akili yake kisha asubiri mtihani.

Akishapewa karatasi za mtihani:

1. Asome maelekezo yote kwa uangalifu kwenye kila ukurasa.

2. Ajibu maswali anayoyaelewa vizuri kwanza. Maswali magumu atayajibu mwisho.

3. Apange muda wa kila swali kuendana na idadi ya maswali anayotakiwa kujibu akizingatia masaa ya mtihani.

4. Kitabu chake cha kujibia mtihani ni kitu muhimu sana, asikichafue au kikilowanisha.

5. Baada ya kumaliza mtihani, ahakikishe amejibu maswali yote anayotakiwa kujibu.

6. Apitie maelekezo yote aliyopewa kwa mara nyingine na ahakikishe amezingatia yote.

7. Mwisho amshukuru Mungu kwa maombi. Kwa sababu alisoma vizuri atafaulu tu.

Nawapenda wote na naamini hayo niliyowaandikia yatawasaidia kwa namna moja au nyingine kwenye mtihani wao.Mungu awabariki [emoji1374]
 
Back
Top Bottom