Kinga mwili ni muhimu sana kwani hutuwezesha kukabiliana na magonjwa. Kwa njia ya kupata muda wa kutosha wa kupumzika tunatoa nafasi kwa mfumo mzima wa kinga mwili kujijenga na kujiimarisha.
Kinga mwili ni muhimu sana kwani hutuwezesha kukabiliana na magonjwa. Kwa njia ya kupata muda wa kutosha wa kupumzika tunatoa nafasi kwa mfumo mzima wa kinga mwili kujijenga na kujiimarisha.
Je ulishasikia ajali zilizosababishwa na madereva wanaosinzia? Uchoovu na kukosa muda wa kupumzika (hasa kulala) humfanya mtu akose utulivu na uwezo wa kumudu chombo anachoedesha.
Hivyo ni muhimu kwa madereva na watu wote wanaotumia vyombo vya usafiri kuhakikisha wanapata muda mzuri na wakutosha wa kupumzika.
Naamini hutopuuzia tena swala la kupumzika kwani umeona jinsi lilivyo na umuhimu mkubwa. Kumbuka kuwa ili uwe na ufanisi mzuri katika kazi au kile unachokifanya unahitaji kuhakikisha mwili na akili yako viko katika hali nzuri. Je wewe huwa unapumzika? Acha kuchakaza mwili wako sasa; tenga muda wa kutosha wa kupumzika.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.