Hakuna asiyejua kuwa nyota wa Manchester United, Paul Pogba kwa sasa hapatani na kocha wake, Jose Mourinho, lakini kitu ambacho wengi hawakijui ni kwamba mchezaji huyo atabaki katika kikosi hicho kwa muda mrefu ama anaondoka.
Lakini, mwenyewe ameweka wazi kwamba huenda akatua zake Barcelona kauli ambayo ameitoa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Nyota huyo alipoulizwa juu ya jambo hilo alisema: "Kwa sasa nacheza Manchester United, lakini nani anajua kesho yangu, Barcelona ni timu nzuri na wachezaji wengi wanaipenda.”
“Niwaambie kitu kimoja, kwa sasa sijavaa jezi ya Barca kwa hiyo zitabaki kuwa tetesi tu, lakini nasisitiza hakuna ajuaye ya kesho.”