SIMAMA KATIKA NAFASI YAKO, MUNGU
ANAMAKUSUDI NA WEWE
Ni wewe pekee mwenye kujua magumu
unayoyapitia na uzito wa changamoto
unazokumbana nazo katika maisha. Ni wewe
pekee mwenye maelazo na lugha sahihi ya
kumueleza Mungu juu ya shida zako, usikatishwe
tamaa.
Usinyamazishwe na watu ambao hawajui historia
yako, hawajui shida yako, hawajui maumivu yako,
na hawajawahi kuyapitia magumu yanayokusonga
wala mazingira yako.
Ilikua rahisi watu kumnyamazisha Batimayo kwa
sababu walikua hawajui nini maana ya UPOFU
=>Usinyamazishwe na watu ambao wana wazazi
wao kwa kuwa hawajui nini maana ya kuwa
YATIMA
=>Usinyamazishwe na watu ambao wako kwenye
ndoa zao na hawajui nini maana ya kuachwa/
kutelelekezwa, ujane /ugane, au kutalakiwa.
=>Usinyamazishwe na wale walio na watoto na
hawajui ugumu, maumivu ya kutokuzaa watoto
=>Usinyamazishwe na wale walio na wenzi
waaminifu na hawajui nini maana ya kusalitiwa.
=>Usinyamazishwe na wale walio na kazi na
hawajui ugumu wa kutafuta kazi miaka na miaka
bila mafanikio.
=>Usinyamazishwe na wale walio na watoto
waaminifu/wasikivu na hawajui nini maana ya
kuwa na watoto wakaidi, waasi, watukutu,
walioshindikana.
=>Usinyamazishwe na watu ambao
wameshafanikiwa kimaisha na hawajui ugumu au
shida ya kuwa masikini.
=>Usinyamazishwe na wale wenye uwezo wakula
Milo mitatu ya maana kwakuwa hawajui nini
maana ya kulala na njaa
Wewe ndiye unajua uchungu unaoupitia, maumivu
na upweke unajua wewe mwenyewe, kama
Batimayo alivyoipaza sauti kwa Yesu, Endelea
kuita na Yesu atakusikia hakika!
Nakutia moyo ya kwamba Mungu Yupo na ndiye
mwenye usemi wa mwisho juu ya maisha yako.
USIOGOPE Yeye sio kipofu hata asione machozi
yako, yeye sio kiziwi asisikie maombi yako, na
hajakaa kimya kwa maumivu yako, Anajua,
Anaona , anasikia atakutendea vyema hakika kwa
majira na wakati unaofaa!
Mungu akutie nguvu kusimama!
Bwana akutendee vyema.
Uwe na Siku njema ya mapambano dhidi ya
mafanikio