Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hatimaye mshambuliaji ghali wa Juventus, Cristiano Ronaldo amemaliza ukame wa mabao kwa kufunga kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu Italia ‘Serie A’ huku akiweka rekodi ya kufikisha mabao 400.

Ronaldo alifunga bao hilo katika dakika ya tano ya kipindi cha pili Juventus ilipoikaribisha Sassuolo kwenye uwanja wa Allianz na Juventus kushinda kwa mabao 2-1.

Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa ada ya uhamisho ya Euro 100 milioni akitokea Real Madrid, Julai mwaka huu, aliongeza bao la pili dakika tano baadaye na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo kupagawa kwa furaha.

Furaha ya mashabiki hao ilitokana na mshambuliaji huyo wa Ureno kushindwa kufunga bao katika michezo mitatu ya kwanza ya Serie A ingawa timu yake ilishinda mechi zote.
 
Kabla ya mchezo huo kuanza, Kocha Massimiliano Allegri, alisema muda wa mshambuliaji huyo kufunga umefika na kwamba mashabiki wajiandae kufurahia mabao yake, ingawa Kocha huyo hakukusudia katika Seria A bali alimaanisha Ronaldo ataifungia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Timu ya Sassuolo ambayo msimu huu imeonyesha kuwa moto wa kuotea mbali ilionyesha upambanaji wake baada ya kupata bao la kufutia machozi katika dakika za majeruhi mfungaji akiwa Khouma Babacar.

"Tangu siku ya kwanza nimefika hapa nilikuwa natamani kufunga, ingawa timu ilikuwa inashinda lakini, nililisubiri bao langu la kwanza kwa hamu kubwa leo hii nina furaha kuu kupata bao naamini mashabiki pia wamefurahia sana,” alisema Ronaldo.
 
Alisema ingawa amezoea maisha ya kushutumiwa na mashabiki, lakini alikuwa akijisikia vibaya sana kutopata bao katika mechi tatu za kwanza za Ligi Kuu Italia.

Ronaldo anasubiriwa kwa hamu kubwa kuiongoza Juventus keshokutwa Jumatano katika mchezo wa kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya watakapoifuata Valencia ya Hispania.

Kiu ya kutwaa taji la Ligi Mabingwa Ulaya ndiyo iliyowasukuma Juventus kumsajili Ronaldo, ambaye ametwaa taji hilo mara tano ikiwemo kuipa Real Madrid ubingwa huo mara tatu mfululizo katika maisha yake ya mwisho Santiago Bernabeu.

Juventus haijatwaa ubingwa huo tangu mwaka 1996 na inaamini kwa uwezo binafsi Ronaldo ataipa ubingwa huo mwaka huu.
 
Wachezaji wa Flamengo na Vasco da Gama walisahau tofauti zao kwa muda na kumsaidia mchezaji mwenzao aliyekuwa ameumia, lakini gari la kubeba wagonjwa lililombeba kumkimbiza hospitali liligoma kuwaka uwanjani.

Mchezaji wa Vasco, Bruno Silva aliumia katika kipindi cha pili na kuhitaji msaada wa gari la wagonjwa ‘ambulance’ kuingia uwanjani kumchukua.

Hata hivyo, baada ya mchezaji huyo kuingizwa katika gari hilo, liligoma kuwaka likiwa ndani ya uwanja.
 
Kutokana na tukio hilo mashabiki 54,000, waliokuwepo kwenye Uwanja wa Mane Garrincha walianza kuzomea ndipo wachezaji wa timu hizo walipoamua kuchukua jukumu la kuisukuma gari hiyo hadi kuwaka.

Baada ya gari hilo kuwaka lilimchukua Bruno Silva hadi hospitali alipolazwa na kuruhusiwa usiku baada ya kupatiwa matibabu.

Pamoja na ushirikiano huo wachezaji, lakini beki wa Flamengo, Rever hakufurahishwa na jinsi wachezaji wenzake walivyolazimika kusukuma gari hilo.
 
Mechi kati ya Vasco na Flamengo wakati wote imekuwa na ushindani mkubwa ndani na nje ya uwanja kutokana na matukio ya vurugu, lakini kwa mara ya kwanza wachezaji wa timu hizo mbili walishirikina.

Katika mchezo huo, Vasco ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika 27, kupitia Andres Rios kabla ya Flamengo kusawazisha kupitia Luiz Gustavo aliyejifunga mwenyewe.

Kiungo wa Flamengo, Diego alitolewa nje kwa kadi nyekundu zikiwa zimebakia dakika 13 mchezo kumalizika. Vasco nao walimaliza wachezaji 10 baada ya kuwatumia wachezaji wake watatu wa akiba kabla ya Silva kuumia na kutolewa nje.
 
A doctor and a lawyer were talking at a party. Their conversation was constantly interrupted by people describing their ailments and asking the doctor for free medical advice.

After an hour of this, the exasperated doctor asked the lawyer, “What do you do to stop people from asking you for legal advice when you’re out of the office?”

“I give it to them,” replied the lawyer, “and then I send them a bill.”

The doctor was shocked, but agreed to give it a try.

The next day, still feeling slightly guilty, the doctor prepared the bills.

When he went to place them in his mailbox, he found a bill from the lawyer.
 
A guy takes a girl on a date. She orders costly champagne, oysters, lobsters, the most expensive food on the menu. The guy asks: “Do you eat like this at your mom’s place?”

The girl replies, “No, my mother doesn’t plan to sleep with me after the meal.’
 
Back
Top Bottom