Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mshambuliaji mahiri na nahodha wa Barcelona, Lion Mess ameendelea kuonyesha miujiza yake katika soka, baada ya jana Jumanne kufunga mabao matatu ‘hat-trick’ ya 48 tangu ameanza kucheza soka.

Mabao hayo aliyafunga katika mechi ya kwanza ya Kundi B ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven ya Uholanzi, yamemfanya Messi raia wa Argentina kuwa mchezaji anayeongoza barani Ulaya kwa kufunga 'hat trick' nyingi zaidi ya wengine.

Mchezaji huyo alianza kufunga bao la kuongoza kwa mpira wa faulo ‘free-kick’ dakika ya 31, ikiwa ni faulo ya nane kwake kufunga kwa mwaka 2018, kabla ya kukamilisha 'hat-trick' ya 42, kwa Barcelona dakika za 77 na 87, ikiwa ni ya nane kwake kwenye michuano ya Ulaya, sita alizifunga kwenye timu ya Taifa ya Argentina.

Aidha Messi ameweza kuifikia rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na nahodha wa zamani wa Real Madrid, Raul kwa kufunga mabao 104 katika michuano ya Ulaya akiwa ameyafunga katika michuano 14 tofauti.
 
IMG-20180907-WA0002.jpg
 
Ushindi huo umeiwezesha Barcelona kushinda mchezo wa 25 kati ya 27 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp, wamepoteza mechi mbili pekee mchezo wa mwisho kufungwa kwenye uwanja huo ulifanyika Mei, 2013, walipofungwa na Bayern Munich mabao 3-0.

Bao jingine la Barcelona katika mchezo wa juzi lilifungwa na winga wao kutoka Ufaransa, Ousmane Dembele, wakati mlinzi Samuel Umtiti alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa mchezo mbaya.
 
Katika mechi zijazo PSV inayonolewa na kiungo wa zamani wa Barcelona, Mark van Bommel, itaikaribisha Inter Milan ya Italia wakati Barcelona itasafiri kuifuata Tottenham.

, Lion Mess ameendelea kuonyesha miujiza yake katika soka, baada ya kufunga mabao matatu ‘hat-trick’ ya 48 tangu ameanza kucheza soka.

Mabao hayo aliyafunga katika mechi ya kwanza ya Kundi B ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven ya Uholanzi, yamemfanya Messi raia wa Argentina kuwa mchezaji anayeongoza barani Ulaya kwa kufunga 'hat trick' nyingi zaidi ya wengine.
 
Mchezaji huyo alianza kufunga bao la kuongoza kwa mpira wa faulo ‘free-kick’ dakika ya 31, ikiwa ni faulo ya nane kwake kufunga kwa mwaka 2018, kabla ya kukamilisha 'hat-trick' ya 42, kwa Barcelona dakika za 77 na 87, ikiwa ni ya nane kwake kwenye michuano ya Ulaya, sita alizifunga kwenye timu ya Taifa ya Argentina.

Aidha Messi ameweza kuifikia rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na nahodha wa zamani wa Real Madrid, Raul kwa kufunga mabao 104 katika michuano ya Ulaya akiwa ameyafunga katika michuano 14 tofauti.
 
Ushindi huo umeiwezesha Barcelona kushinda mchezo wa 25 kati ya 27 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp, wamepoteza mechi mbili pekee mchezo wa mwisho kufungwa kwenye uwanja huo ulifanyika Mei, 2013, walipofungwa na Bayern Munich mabao 3-0.

Bao jingine la Barcelona katika mchezo wa juzi lilifungwa na winga wao kutoka Ufaransa, Ousmane Dembele, wakati mlinzi Samuel Umtiti alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa mchezo mbaya.

Katika mechi zijazo PSV inayonolewa na kiungo wa zamani wa Barcelona, Mark van Bommel, itaikaribisha Inter Milan ya Italia wakati Barcelona itasafiri kuifuata Tottenham.
 
Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair, anapewa nafasi kubwa ya kuwa Mwenyekiti mpya wa bodi inayosimamia Ligi Kuu England ‘Premier League’.

Blair ambaye ni shabiki wa Newcastle United ndiye mtu anayeonekana kuwa sahihi kumrithi, Richard Scudamore ‘1959’, aliyeshika wadhifa huo tangu Juni 2014.

Ingawa wapo wengi wanaotajwa kuwania nafasi hiyo lakini wanaopewa nafasi kubwa baada ya Blair ni bosi wa BT, Gavin Patterson na yule wa Sky Sports, Barney Francis.
 
Ingawa kulikuwa na mijadala mizito baina ya viongozi wa klabu kuhusu uelewa wa Blair katika mambo ya soka lakini baadaye asilimia kubwa ikaridhia kumpa uongozi kutokana na rekodi nzuri ya utendaji wake.

Shabiki huyo wa Newcastle anasubiri kikao cha mwisho cha klabu kitakachoongozwa na kigogo wa Chelsea, Bruce Buck, ili kumuidhinisha kushika wadhifa huo.
 
Ingawa mashabiki wa Tottenham wanasifika kwa utulivu miongoni mwa mashabiki wa timu za England, lakini safari hii uvumilivu umewashinda na wamemjia juu kocha wa timu hiyo, Mauricio Pochettino.

Hicho kilikuwa kipigo cha tatu kwa Spurs msimu huu, walifungwa mabao 2 -1, na Liverpool na Watford katika mechi za Ligi Kuu England vipigo vilivyoirudisha nyuma iliyochezwa Vicarage Road.

Mashabiki hao walikerwa na majibu ya Kocha huyo aliyewaambia yeye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho wa kikosi chake, akiwaambia aulizwe tu kama timu itafungwa lakini si nani atacheza na nani akae benchi.
 
Back
Top Bottom