Wanasoka wote wa kizazi kipya, hasa wale wanaokipiga kwenye Ligi Kuu England wanavutiwa na viwalo hivyo, ambapo kiungo wa Liverpool, Naby Keita ameamua kununua ile ya gharama nafuu kidogo, ambayo imemgharimu Pauni 1,930 ikiwa juu na chini.
Staa wa Tottenham Hotspur, Dele Alli yeye kaptula yake tu Gucci imemgharimu Pauni 670, huku ile ya Lingard ikimgharimu Pauni 870.
Wengi wao wamekuwa wakitupia Gucci kaptula, ambapo kwenye orodha hiyo wapo pia Danny Simpson na Nathaniel Clyne.
Hata hivyo, bei yake imechangamka, huko dukani inauzwa Pauni 670.
Keita alitaka kuonyesha yeye ni matata kabisa kutupia viwalo, ambapo alipiga Gucci juu na chini ilikuwa na kutinga raba ya Ace yenye thamani ya Pauni 630 kumfanya mtoko wake wa mavazi wote kwa siku hiyo ambayo alipigwa picha awe ametupia Pauni 2,600.