Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Jahazi la Simba limeanza kwenda mlama baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Shujaa wa Mbao katika mchezo huo alikuwa Said Khamis mfungaji wa bao pekee la mkwaju wa penalty katika dakika 26 na kuwaacha mabingwa watetezi Simba wakiwa wamedua.
Ushindi huo unaifanya Mbao kuongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 10, wakati Simba ikibaki na pointi zake saba.
Kabla ya mchezo huo Kocha wa Mbao, Amri Said alisema lengo lake ni kuondoa uteja kwao kwa kufungwa zaidi na Simba pamoja na kutopoteza tena mchezo nyumbani.