Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jahazi la Simba limeanza kwenda mlama baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Shujaa wa Mbao katika mchezo huo alikuwa Said Khamis mfungaji wa bao pekee la mkwaju wa penalty katika dakika 26 na kuwaacha mabingwa watetezi Simba wakiwa wamedua.

Ushindi huo unaifanya Mbao kuongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 10, wakati Simba ikibaki na pointi zake saba.

Kabla ya mchezo huo Kocha wa Mbao, Amri Said alisema lengo lake ni kuondoa uteja kwao kwa kufungwa zaidi na Simba pamoja na kutopoteza tena mchezo nyumbani.
 
Alisema kuwa amewaandaa vyema wachezaji kisaikolojia kuhakikisha wanashinda mchezo huo ili kujiweka nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi na kwamba timu ya sasa ni tofauti na misimu iliyopita.

Achana na bao la kuongoza lililofungwa kwa penalti na Said Khamis wa Mbao, lakini utamu wa mechi ulikuwa kwa mshambuliaji Pastory Athanas jinsi alivyokuwa akimkimbiza beki wa Simba, Pascal Wawa.

Katika mchezo huo bao la Mbao lilifungwa kwa mkwaju wa penalti baada ya Aish Manula kumwangusha Athanas katika eneo la hatari alipokuwa anakwenda kufunga.
 
Kipindi cha kwanza Wawa amezidiwa mbinu na mashambulizi huyo wa zamani wa Simba ambaye alishindwa kung'aa na kuamua kuondoka kikosini hapo.

Simba ililishambulia lango la wapinzani wao mara kwa mara, lakini safu yao ya ushambuliaji ilikosa umakini kwani mashambulizi yao hayakuwa na madhara huku mipira yao mingi ilizaa kona.

Kipindi cha kwanza Mbao hawakupata kona hata moja lakini walifanya mashambulizi ya kushitukiza ambayo kwa umahiri wa Manula aliyadhibiti tofauti na wao ambao walifika langoni mwa Mbao mara nyingi pasipo na faida.
 
Kichuya alianza kuchungulia lango la Mbao dakika ya pili tu ya mchezo kwa kupiga kona lakini haikuwa na madhara yoyote huku John Bocco na Emmauel Okwi dakika ya 6 na 13 walipiga mashuti yaliyotoka nje ya lango.

Kipindi cha pili Simba ilijitahidi kupambana ili kupata bao la kusawazisha, lakini ukuta wa Mbao ulionekana kuwa imara zaidi kwa kuzuia mashambulizi.

Makocha wote walifanya mabadiliko ya wachezaji ili kupata matokeo zaidi huku akiwatoa Mohamed Ibrahim nafasi yake ilichukuliwa na Meddie Kagere ambaye alikosa magoli mara tu ya kuingia dakika ya 60, 73 na 81.
 
Bahati haikuwa upande wa Simba kwani Okwi naye alikosa bao dakika ya 63 akipiga shuti lililookolewa na kipa wa Mbao, Hashim Musa ikiwa ni mpira wa faulo.

Aussems katika kupambana alimtoa Kichuya nafasi yake ilichukuliwa na Rashidi Juma huku Amri Saidi naye akifanya mabadiliko kwa kuwatoa Hussein Seleman aliingia Elius Zamfuko, alitoka Rajesh Kotecha nafasi yake ilikwenda kwa Evarist Mujwahuki wote kipindi cha pili pamoja na Abubakar Mfaume huku Rolland Msonjo akiingia.
 
Kocha wa Mbao kipindi cha pili alionekana kucheza zaidi kwa kulinda bao huku Simba walipambana kusawazisha pasipo mafanikio.

Dakika za lala salama Bocco alipiga mpira uliopaa juu ya goli huku Mbao nao walijibu mapigo hayo kwa kupiga shuti ambalo pia lilipaa juu ya goli.

Simba leo Alhamis wataanza safari ya kwenda Shinyanga kucheza na Mwadui wakiwa wamepoteza mechi hiyo.
 
Hii ni kwa ajili yako unapokuwa unahisi kukata tamaa ; Siku ambazo unatafuta pa kuficha kichwa chako na kisionekane tena. hii ni kwa ajili yako wakati mashaka yanapofunga mwanga usionekane, wakati unapoona Dunia imekutupa.

Hii ni kwa ajili yako wakati ambapo siku sio nzuri na kila kitu hakiendi vizuri… unaposhindwa, unapozama, unapojikuna kwenye ngozi yako ya kichwa, na hujui kama utaweza kuendelea.

Wakati mwingine maisha yanakuwa magumu kupita kiasi… ni magumu kuliko unavyofikiria. magumu kuliko ulivyotegemea. kuna siku ambazo zinakuweka kitandani. siku za majaribu makubwa.
 
Huenda unafikiri maisha ni mazito sana; kama vile huwezi kuishi. Unaweza kufikiri Ulimwengu wote umekuelemea mabegani,umekuondolea nguvu, unakusukuma chini pamoja na roho yako. Kila sehemu ya mwili wako una maumivu. huwezi kabisa mahali hapo.

Hakuna kitu sahihi. Hata kama unajua kuwa una masikitiko, hivyo huna kitu, huwezi kuweka kidole chako. huwezi kusema hisia hizo. lakini unajua unajisikiaje.

Unaweza kusikia kama kukata tamaa. unaweza kusikia huna kitu…Umechoka…imefanyika.lakini lazima usubiri. lazima utafute kitu cha kukusimamisha hata kidogo, na hicho kitu kikuhudumie wakati huo. unaweza kushikilia kwa muda mrefu uwezavyo. usiachie.

Inaweza kuwa kitu chako kikubwa cha kufanya ni kupumua na kuvuta hewa, ili uweze kutoka kitandani. Na unafahamu ni kitu gani? Huenda hio ni sawa. endelea kupumua , ndani na nje, vuta hewa ndani , shikilia kwa muda halafu pumua nje. utajisikia vizuri.
 
Huenda unafikiri kuwa umevunjika sana na huwezi kutengamaa; kwamba maumivu hayo ndani ya moyo wako yamekaa. kwamba akili yako imeharibika, na umeathiriwa kabisa. Lakini nakuambia hivi, chukua hilo moyoni na anza kusema mwili wako ni imara. Mwili wako unafahamu jinsi ya kuponya.

Hutaweza kuwa na hali ya kuvunjika moja kwa moja. kila siku unaweza kuanza tena, na kila siku utakuwa na badiliko la kuweka mambo pamoja. inaweza kuchukua muda mrefu na inaweza kuhitaji nguvu,lakini hujavunjika. umepitia kwenye mlima mrefu kidogo. hakuna kitu kinachoweza kudumu katika Ulimwengu huu. hakuna kitu kinachoweza kubaki kile kile bila ya kubadilika . hata nyakati mbaya zinapita, hisia mbaya zinapita. kwa hio nakusihi kaa nazo nakuhakikishia ipo nafasi mpya. utajisikia vizuri hivi karibuni. na utakapoanza kupona tena , utaona sehemu zako zilizovunjika zinapona na kuwa na nguvu. masikitiko sio dalili ya udhaifu.
 
Ruhusu nafasi ya kupumua, na uelewe kuwa yale maisha yalikuwa ni maisha kama mengine. ni sawa kukosea. ni sawa kushuka chini. ni sawa kujisikia vibaya …hata zaidi , mbaya zaidi ,nafahamu hivi sasa inaoneka una maumivu na hayaishi, lakini huenda huu ni mwanzo wa kitu tofauti. ni sawa kuanguka wakati mwingine, kwa sababu hata wakati unafanya , hutakaa hapo kwa muda mrefu.

Hauhitaji kukataa hisia zako au kuzisukumia mbali kwa maumivu. acha maumivu yakupate, ili huenda unaweza kuelewa kwamba zilikuwa ni wageni ,hazikuja kukaa.

Badala yake, Fahamu kwamba kuhisi kwako vibaya sio sababu ya kupunguza maumivu.
 
Lakini pia tambua kwamba akili yako ina njia ya kukunja ukweli; akili yako ina njia ya kukuongoza kuamini kwamba kukosa usalama kwako na woga unapata nguvu.. Usisikilize sauti hio. tambua kwamba akili yako inadanganya, na kwa kufanya hivyo kuwa makini unapochagua ni mawazo gani yapo sahihi ambayo unaweza kuamini.

Kama utakubali mahali ulipo sasa katika maisha yako. na kukubali kuwa baadae mambo yatakuwa mazuri, ni bora kuliko kuogopa. utaanza kuona kwamba hata kama uko gizani mwanga lazima utakuja kwako. hata kama unahisi kupotea na kuchanganyikiwa au kama ulimwengu umezidi magumu. kaa na hisia zako , na chukulia kwa taratibu kila jambo na kwa urahisi.

Tafuta kitu kidogo sana ambacho kinakufanya utabasamu, na sogea mahali ulipo. hatua ndogo. Kama utaanza njia yako ndogo, kila kitu kitaanza kurudi sehemu yake. Omba msaada kama unahitaji, na jifunze kwa wengine kama utahitaji kufanya hivyo. nafasi zipo. Watu wanakutaka uwe na furaha kwa sababu wanakupenda . kwa hio kuwa wazi , uwe mwanga kwa wengine, wafanye wengine waishi wakati unapojisikia uko chini.
 
Pumua ndani na nje. upo hapa, una mambo mengi mazuri kichwani mwako. hisia nzuri moyoni mwako– unatakiwa tu kutazama ndani zaidi kushukuru siku ya leo. jaribu kutosahau vitu vyote vizuri ndani yako.

Hata kama umeumia, Bado ni wewe. Na utakapokuwa tayari kutafuta vizuri vyote, vitakuwa vinakusubiri.
 
Usisahau kwamba hata kama Ulimwengu umegeuka upande mwingine bado unao uwezo wa kujiokoa . una uwezo wa kutengeneza daraja juu ya bahari, maji yasiofahamika. unaweza kupita kati ya giza na kukutana na mwanga tena. unaweza kusonga mbele. Mambo yatakuwa mazuri kwa muda wake.

Kwa hio jinsi unavyosonga mbele , Natumaini utakutana na baraka zako kila hatua . inaweza kuchukua muda mrefu. lakini ipo siku utaona mwanga tena.

Unacho kitu kikubwa ambacho hakuna mtu wa kukifanya katika ulimwengu huu, una miujiza yako mwenyewe, utambulisho wako, ukweli wako, na njia yako ya upekee ya kusambaza upendo na huruma kwa watu.

Wewe ni mwezi, jua, Mwanga, giza, nyota, mlima, wewe ni ulimwengu wote, unatawala mwelekeo wote. chini na juu. wewe ni wa kweli.

Vuta pumzi ndani na kutoa nje. Utakuwa vizuri.
 
*NIMEUMIA SANA*

*Ameandika Rashid chilumba*
Nimesikia zoezi la uokoaji kwenye ajali ya kivuko Mwanza limesitishwa hadi kesho kutokana na kiza, sasa kesho mtakwenda kuokoa au kuokota Maiti?

Hapo Mwanza kuna kikosi cha Jeshi, boti za doria za polisi, helikopta na vivuko vingine? Hivi kweli vyote hivyo havina taa kubwa za kuwezesha zoezi la uokozi kuendelea usiku kucha? Kama havina tulivinunua vya kazi gani?

Ni aibu kwa viongozi kusema tunaenda kulala eti kuna giza ziwani wakati kuna dazani ya watanzania wenzetu tunaowahudumia wamezama ziwani tena siyo kwa uzembe wao bali kwa ujuba na tabia ya kutokujali maisha ya watu na kusimamia usalama wao.

Mkuu wa mkoa, RPC, mkuu wa kamandi ya Jeshi la Wananchi, Mkuu wa Bandari Mwanza mnapata wapi ujasiri wa kwenda kulala na kuna watu watoto wao, baba zao, Mama zao wamo majini na hawajui kama watawapata wakiwa hai? Hivi ingelikuwa ni jamaa zenu wa karibu mngepata ujasiri wa kusimamisha zoezi kwa sababu ya kiza?

Katika dunia ya leo seriously kabisa mnasema kiza kinawazuia kuokoa watu? Aiseee.... Kwa hiyo hao waliozama ikiwa kwa bahati bado wapo hao hadi sasa mnategemea Israeli atawangoja ninyi hadi kesho jua litapochomoza? Huu ni uzembe wa hali ya juu mno.

Kweli kabisa mnashindwa kufunga tochi kubwa kama zile za bandari kwenye helikopta moja ya polisi hapo na boti nne tano mkaingia kuwaokoa watanzania wenzetu? Hata ikiwa ni wafu lakini faraja ni kupata japo miili yao hadi kesho samaki, mawimbi ya ziwa nk inaweza kuwa imewapoteza zaidi.

Leo nimeumia sana, makosa yale yake ya Mv Bukoba, Spice Islander, Skagit yamejirudia Mv. Nyerere na watu wanaenda kulala usiku umeingia na vyombo vya habari vinaonesha shilawadu na kutoa dakika kiduchu kwa habari muhimu na msiba mkubwa huo wa taifa.

Na tena mlionywa mara kadhaa kuwa chombo ni kibovu. Mkuu wa bandari ya mwanza bado yupo na wadhifa wake na msimamizi wa Sumatra kanda ya ziwa kesho ataenda pia ofisini.

Mungu awapumzishe waliotangulia na atawalipa waliowasababishia kuzama kwenu kwa uzembe wao.
 
so sad
 
You will know your Guy is ready to be a FATHER when he holds both your legs up during SEX like he is changing pampers....[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Don't ask me how i know i just know.[emoji135][emoji135]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…