Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mitandao inakuambia jinsi gani unatakiwa kuishi na jinsi gani hutakiwi kuishi. yapo makosa unaweza kufanya , kama hutaelewa vizuri. Mengine yanaweza kukuongoza na mengine kukupoteza

Unaweza kukutana na njia ambayo ni nzuri ambayo hata mwandishi aliyekuambia hajawahi kupitia njia hio. Au unaweza kukutana na njia isiyo sahihi kutokana na jinsi ulivyoelewa wewe. Ni vizuri kuwa na hekima kuchukua ushauri mzuri na kuufanyia kazi. Wengi huishia kwenye theory lakini vitendo ni ziro.

Kwa hapa nakuelezea jinsi ya kutumia maisha yako yaliobaki ili usije kujilaumu baadae.
 
Nipo hapa kusema kuwa hatujui kila kitu. lakini kile kidogo ambacho tunakijua ndicho tunachokupa wewe. kwa hio usijikatae katika maisha yako. jikubali kwa kila kitu unachokifanya. kubali mawazo yako.

Utaweza kupata maana utakapo pata kwenye vitabu, kutoka kwa mtu, ndio , huenda ni moja ya makala ikakupa kitu kizuri na ukakifanyia kazi . huenda ndio hii ambayo najaribu kukuweka sawa sasa. ni sahihi , na ni nzuri, kusema kweli. kwa sababu tunachagua msukumo wakati tunapohitaji. tunachukua chenye sababu.

Lakini usitake kusema maisha yako yameharibika kwa sababu umekosana na mwenza wako, umeachwa, umeumizwa. hutakiwi kufikiria kuwa umeharibu maisha yako. badala yake tambua kuwa umejifunza, umepata uzoefu wa maisha. Hujaharibu maisha kwa sababu umecheza kwa usalama. hujaharibu maisha yako kwa sababu umechanua tofauti kuliko unavyoamini. hujaharibu maisha yako kwa sababu umekwisha kutatua.
 
Kwa nini?

Kwa sababu hakuna kitu kama hicho cha kuharibu maisha.

Kusema hivyo ni kujishusha thamani, katika maisha mara milioni.

Nia , ndoto zinabadilika. Na sio tu kwa sababu kitu ulichokitaka kitokee hakikutokea haina maana kwamba maisha yameharibika.

Utakuwepo muda katika maisha yako , wakati ambao utasikiliza maoni ya wengine zaidi kuliko kusikiliza moyo wako mwenyewe. Huo wakati utakuwa kimya badala ya kuongea kwenye akili yako. wakati huo utakosa nafasi . ndipo hapo utakutana na lawama ndani yako.

Kutakuwepo na makosa, na kushindwa. Kwa sababu wewe ni mwanadamu. kwa sababu kuna ubaya na uzuri na hakuna uwezekano wa kujua jinsi gani utaishi maisha yako.
 
Maisha ni yako tu na ndiyo uliyonayo. kuna siku unaweza kujisikia vizuri na kuna wakati utajisikia vibaya. Ni sawa kulia au kuchanganyikiwa wakati mwingine. katika siku ambazo utaona ushindi usio na mwisho , furahia. Jaribu kukumbuka kila kitu ambacho sio cha kudumu milele. Kila kitu kinakuja na kuondoka.

Kitu pekee ambacho kinaharibu maisha yako ni kuamini kuwa umefanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…