Tabia ya kutozingatia vitu vya msingi inazidi kushika kasi miongoni mwa watu walio wengi, sio tu katika maswala ya Kisiasa na Elimu bali hata katika maswala ya msingi yahusuyo Afya. Mitazamo duni ya kimaisha inafanya wengi kuyachukulia mambo ya msingi kiuwepesi na matokeo yake wengi huishia kulia na kulaumu.
Katika uwanja wa Afya, tabia ya matumizi ya dawa za muhimu bila kufata maelekezo inazidi kushamili licha ya msisitizo uliopo juu ya matumizi sahihi ya dawa. Maelekezo yamekua yakitolewa na wahudumu wa Afya sambamba na zoezi na ugawaji dawa, maelekezo kama “tumia dawa mara tatu kwa siku kwa muda wa siku saba, tumia maji mengi unywapo dawa, kula vizuri kabla ya kunywa dawa na usiingie kulala mara baada tu ya kunywa dawa” hutolewa yakiwa na maana kubwa sana na kila mtu anapaswa kuzingatia ili kuboresha Afya, lakini walio wengine hawayazingatii.