Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1537548391685.jpg
 
Ni kawaida kwa binadamu kupatwa na maumivu au maradhi madogo madogo mara kwa mara hasa watoto wadogo. Dalili nyingi huanza wakati tusiotarajia na pengine tunashindwa kuapata msaada wa haraka. Haya baadhi ya mapendekezo ya dawa ambazo yafaa kuwa nazo nyumbani zikusaidie wakati wa shida au dharura
 
Zingatia!!!
Kabla ya kutumia dawa, daima usome lebo ya pakiti na kipeperushi ndani ya pakiti. Hii ni kwa ajili ya maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa na juu ya nani asiyepaswa kutumia dawa hii pia kwa orodha ya madhara yanayoweza kusababishwa na dawa(side effects).
Weka dawa mbali na watoto.
Wajawazito waepuke sana kutumia dawa bila maelekezo ya daktari kwani baadhi ya dawa humdhuru mtoto tumboni.
 
Paracetamol (panadol)

Paracetamol hutuliza maumivu na homa. Inapatikana kwa njia ya vidonge kwa watu wazima na majimaji kwa watoto wadogo. Ikiwa una watoto wadogo, paracetamol yaweza kuwa ni dawa muhimu kuliko zote kwako. Paracetamol ni salama kwa kiwango cha kawaida lakini ni hatari unapokunywa nyingi mno (overdose).
 
Dawa za kutuliza maumivu za Anti-inflammatory

Hizi ni dawa za kutuliza maumivu ambazo pia hupunguza kuvimba. Husaidia kwa maumivu ya misuli na vidonda, maumivu ya hedhi na pia hushusha homa. Kunywa dawa hizi pamoja na chakula kuepusha vidonda vya tumbo. m.f. Ibuprofen, Aspirin, Naproxen
 
Antihistamini.

Hizi hupunguza dalili zote za aleji -m.f. Aleji za ngozi(urticaria), kuwahswa, kupiga chafya, kutokwa na machozi mno, mafua makali, n.k. Inaweza pia kutumika kutuliza maumivu na uvimbe kwa aliyengatwa na nyuki, dondora, na wadudu mbalimbali.
Antihistamini zingine zinaweza kusababisha usingizi m.f. chlorphenamine(Piriton®), diphenhydramine. Hizi unashauriwa kutumia zaidi usiku. Na ambazo hazileti sana usingizi - m.f. loratadine na cetirizine zinafaa kutumika mchana.
Antihistamine pia hupatikana kama cream, ambayo unaweza kupaka sehemu uliyong’atwa
 
Dawa za kuzuia kuharisha.

Kuharisha huisha kwenyewe mara nyingi lakini inapozidi waweza kutumia dawa zifuatazo Loperamide(Imodium), Pepto-Bismol, Kaopectate, n.k.
Dawa hizi ni zaidi kwa ajili kutuliza maumivu na kutuliza dalili za ugonjwa. Muone daktari kwa ajili ya kupata tiba kamili hasa ukijikuta unahitaji kutumia dawa hizi mara kwa mara. Dalili huweza kuwa ishara ya ugonjwa mkubwa zaidi unaendelea kushamiri mwilini mwako.
 
Back
Top Bottom