Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

zari alishikiliwa airport akauliza sabau akaambiwa kwamba kunamtu alipiga simu UK airport akatoa taarifa kwamba zari anaingia huko kufanya biashara HARAMU na hana hata viza kwahiyo alipoingia tu wakamshikilia kwa masaa kadhaa wakamhoji na kumpekua lakini mwisho wa siku wakakuta kilakitu kipo sawa wakamuachia. . Shigaangu kule wa kushakiza watu wamreport Chibu amepost kujisifia kwqmba niyeye ndo amecheza huo mchezo na hiyo ni kukomoa team zari kwakua wanamuaibisha PUGI.......😜😜😜shouger nakuhurumia uwe niwewe kweli kama usemavyo au usiwe wewe unazuga tu ila UNA HASARA tena KUBWA
41783473_251356135439389_4204849056248229070_n.jpg
 
Mshambuliaji mahiri wa Argentina, Sergio Aguero amesaini mktaba wa mwaka mmoja zaidi kuitumikia Manchester City.

Mchezaji huyo mwenye miaka 30, mkataba wake wa sasa utamalizika mwaka 2020 na kwa kuongeza mwaka mmoja zaidi inamaana atakaa Etihadi hadi 2021.

Aguero, alisajiliwa na City mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid ya Hispania kwa ada ya Pauni 38 milioni.

Ametwaa mataji matatu ya Ligi Kuu England na matatu ya Kombe la Ligi, kwa sasa ndiye anayeshikilia rekodi ya mabao katika klabu hiyo akiwa amefunga mabao 204 likiwemo bao la dakika za majeruhi dhidi ya QPR lililoipa ubingwa wa kwanza mwaka 2012.
 
Ametwaa mataji matatu ya Ligi Kuu England na matatu ya Kombe la Ligi, kwa sasa ndiye anayeshikilia rekodi ya mabao katika klabu hiyo akiwa amefunga mabao 204 likiwemo bao la dakika za majeruhi dhidi ya QPR lililoipa ubingwa wa kwanza mwaka 2012.

"NInayo furaha sana kuongeza mkataba wa mwaka mmoja, tangu siku ninahamia hapa malengo yangu yalikuwa kukaa hapa kwa miaka kumi na sasa ni wazi ndoto yangu inatimia,” alisema Aguero.
 
KOCHA Unai Emery amesema kitu anachokiwaza kwa sasa ni kuipa Arsenal ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Arsenal imeonakana kuanza na makali kwenye ligi baada ya kushinda mechi mfululizo na usiku wa juzi Alhamisi iliichapa pia FC Vorskla kwenye Europa League uwanjani Emirates.

Emery ambaye ametua Arsenal kuchukua mikoba ya Arsene Wenger amekiri Ligi Kuu England ni tamu kuliko michuano mingine yote ya Ulaya.

“Nimewaambia wachezaji wangu kitu hiki hiki ninachowaambia nyie,” alisema Emery.
 
“Ligi Kuu England ni kitu cha kwanza kwa sababu itatufanya kuwa na heshima zaidi katika msimu. Kila mechi ina utamu wake na nataka wachezaji wangu wawe na moto wakati wote.”

Arsenal itashuka uwanjani kesho Jumapili kumenyana na Everton huko Everton. Wapinzani wao wa London, Chelsea nao watacheza hiyo kesho, lakini wao watakuwa ugenini kwa wababe wengine wa jiji hilo, West Ham United.
 
MWANAFUNZI DARASA LA TATU APEWA MIMBA.
SERIKALI YAAGIZA WAZAZI WAKE WAKAMATWE.

Serikali wilayani Nkasi mkoani Rukwa, imeagiza kukamatwa kwa wazazi wa mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mkinga aliyepata ujauzito kwa kosa la kuandaa mpango wa kumuoza mwanafunzi huyo.

Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mtanda, wakati akikabidhi pikipiki 28 zenye thamani ya Sh. milioni 98 zilizotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, kwa kushirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya mpango wa kukuza stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu kwa waratibu kata wa wilaya hiyo.

Alisema katika kijiji cha Mkinga kuna mwanafunzi wa darasa la tatu amepata ujauzito na wazazi wake walikuwa wanaandaa mkakati wa kumuozesha, lakini walishindwa baada ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kuingilia kati na kuvuruga mpango huo.

"Naagiza wazazi wote wa mwanafunzi huyo wakamatwe mara moja, mwanafunzi huyo pamoja na aliyempa mimba wafikishwe katika vyombo vya dola, ili sheria ichukue mkondo wake na ninyi waratibu elimu kata tambueni mna jukumu kubwa la kuhakikisha mimba hizi zinakwisha, " alisema.

Mtanda alisema hali hiyo inaonyesha kuwa bado tatizo la mimba ni kubwa kwa sababu katika mwezi uliopita jumla ya wanafunzi 27 walipata ujauzito, hivyo bado kuna kazi kubwa ya kufanya.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Misana Kwangula, alisema lengo la serikali kuwapatia pikipiki hizo ni kuwawezesha kutembelea shule zilizopo katika kata zao kwa kuwa walikuwa wanalalamika kuwa hawana vitendea kazi vya kuwawezesha kufanya ukaguzi katika shule wanazozisimamia.
 
Back
Top Bottom