REKODI KUMI ZA KIJINGA ZAIDI ZILIZOPO KWENYE KITABU CHA REKODI CHA “GUINNESS”
1.Vijiko Vingi zaidi kwenye mwili wa Binadamu.
Disemba 28 mwaka 2013, Etibar Elchiyev aliweka vijiko 53 mwilini mwake akiwa amesimama wima na kuvunja rekodi yake mwenyewe!
2.Mtu aliyeolewa mara nyingi zaidi!
Linda Lou Taylor wa jimbo la Indiana nchini marekani, anashikilia rekodi ya kuolewa mara nyingi zaidi akiwa ameolewa mara 23!. Ana miaka 69 kwa sasa na amekuwa akisisitiza kutaka kuolewa kwani hana mpenzi kwa zaidi ya miaka kumi sasa!
3.Watu wengi zaidi Kupiga Mswaki kwa wakati mmoja.
Katika mji wa Manila Nchini Philippines, wanafunzi 10,800 walikusanyika pamoja kupiga mswaki na kutema kwenye kikombe kwa wakati mmoja!
4.Mbwa aliyebeba glass na kutembea umbali Mrefu zaidi.
Usishangae! Wanyama nao wamo. Mmbwa mmoja wa Australia anashikilia rekodi ya kutembea hatua kumi mbele na hatua kumi nyuma akiwa na glass ya maji kichwani!
5.Nywele Ndefu zaidi za Masikioni.
Agosti 26 mwaka 2007, Anthony Victor wa Maduri India, aliweka rekodi ya dunia kuwa binadamu mwenye nywele ndefu zaidi za masikioni zikiwa zimefikia nchi 7!