Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MALEZI HAYA NDIO YAMETENGENEZA VIONGOZI TULIONAO SASA! (UTAWALAUMU?)

Kama umezaliwa kabla ya mwaka 1990 utakubaliana na mimi kwa aina hii ya malezi uliyolelewa nayo!

1.Mzazi ndiye Mungu, yaani hata kama umefundishwa kwamba anga ni la bluu, mzazi akikuambia anga lina rangi ya njano inabidi ukubali!
(matokeo yake viongozi hawakotayari kukosolewa)

2. Nyumbani ni kwa ajili ya yeyote ilimradi tu awe ni ndugu, ndugu yeyote anaweza kuja kukaa kwa muda wowote hata kama alifukuzwa kwao hukuna haja ya kuwa na wasiwasi nae maadam ni ndugu yetu!
(matokeo yake, mgeni toka nje akija, No problem! Ni rafiki zetu sana hawa, mpe ardhi)

3.Mdogo kwenye familia ndiye atakaesingiziwa kafanya uharibifu wowote nyumbani, mpaka atakapokuwa na uwezo wa kujitetea!
(Matokeo yake wenye vyeo wakitaka “kula” wanatumia mgongo wa watu Fulani wa chini ambao hawana sauti)
 
Sababu Zingine

4. Mkubwa kwenye familia ndiye atakaeadhibiwa na kupewa lawama kwa kile mdogo alichofanya mdogo anaachwa.

5. Wazazi watakuita ukiwa nje unacheza, au unasoma ili wakutume uwachukulie kitu kilichopo mita chache kutoka walipokaa.

6. Sahau Suala la kusifiwa, Ukipata B darasani utaambiwa kwani aliyepata A ana vichwa vingapi?

7. Mtoto hafundishwi elimu ya uhusiano anapobalehe. Yeyote anayeonekana nae huitwa rafiki na mzazi hana muda wa kufuatilia. Unachoambiwa ni “Usituletee aibu nyumbani”

8. Mtoto wa kike hafundishwi chochote kuhusu maisha na baba! Mpaka awepo mama au shangazi

9. Kuna Kinywaji Kabatini? Au Kuna kuku anachinjwa? Oooh basi ujue leo kuna mgeni anakuja!


10. Lazima usomee kozi aliyosomea Yule msomi wa kijijini kwenu. Hii ni amri imetoka kwa baba
 
REKODI KUMI ZA KIJINGA ZAIDI ZILIZOPO KWENYE KITABU CHA REKODI CHA “GUINNESS”

1.Vijiko Vingi zaidi kwenye mwili wa Binadamu.
Disemba 28 mwaka 2013, Etibar Elchiyev aliweka vijiko 53 mwilini mwake akiwa amesimama wima na kuvunja rekodi yake mwenyewe!













2.Mtu aliyeolewa mara nyingi zaidi!
Linda Lou Taylor wa jimbo la Indiana nchini marekani, anashikilia rekodi ya kuolewa mara nyingi zaidi akiwa ameolewa mara 23!. Ana miaka 69 kwa sasa na amekuwa akisisitiza kutaka kuolewa kwani hana mpenzi kwa zaidi ya miaka kumi sasa!









3.Watu wengi zaidi Kupiga Mswaki kwa wakati mmoja.
Katika mji wa Manila Nchini Philippines, wanafunzi 10,800 walikusanyika pamoja kupiga mswaki na kutema kwenye kikombe kwa wakati mmoja!












4.Mbwa aliyebeba glass na kutembea umbali Mrefu zaidi.
Usishangae! Wanyama nao wamo. Mmbwa mmoja wa Australia anashikilia rekodi ya kutembea hatua kumi mbele na hatua kumi nyuma akiwa na glass ya maji kichwani!










5.Nywele Ndefu zaidi za Masikioni.
Agosti 26 mwaka 2007, Anthony Victor wa Maduri India, aliweka rekodi ya dunia kuwa binadamu mwenye nywele ndefu zaidi za masikioni zikiwa zimefikia nchi 7!
 
6.Kupigwa Teke Sehemu za siri (mwanaume) kwa spidi ya kilometa 40 kwa saa.
Kirby Roy aliweka rekodi hii alipokubali kupigwa teke zito na mwanamieleka Justice Smith kwa kasi ya kilometa 40 kwa saa teke hilo likiwa na nguvu ya kusogeza kilo mia tano!













7. Choo chenye Kasi zaidi Duniani
Unapoteza muda mwingi kukaa chooni? Colin Furze alitengeneza choo cha kukaa chenye uwezo wa kutembea kwa kasi ya kilometa 100 kwa saa chenye uwezo wa kuflashi!







8.Kuongezeka Uzito kwa kasi zaidi.
Rekodi hii imewekwa na Donna Simpson wa New Jersey, USA. Alifikisha kilo 273.5 kutoka kilo tisini tu! Zoezi hilo alilifanya kwa kipindi cha miaka miwili (2) tu! Alikuwa akitumia zaidi ya shilingi milioni moja kwa wiki kwa kula tu!









9.Mayai Mengi zaidi kupasuliwa kwa kichwa kwa wakati mmoja.
Ashrita Furman anashikilia rekodi ya kupasua mayai 80 kwa kichwa kwa wakati mmoja!











10.Chapati Kubwa Zaidi kutengenezwa!

October 8 2010, katika nchi ya Uturuki, wapishi zaidi ya 50 walikusanyika kwa pamoja na kutengeneza chapatti ya mayai yenye uzito wa tani 6 (Uzito wa gari kubwa). Chapatti hiyo ilichanganywa mafuta lita mia nne (400), na Mayai zaidi ya laki moja (100,000)
 
Back
Top Bottom