Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

2390f375-1e7a-4729-9ca4-9e9c97f29c1e.jpeg
 
Siku tano baada ya mtoto Beauty Yohana (3), kuibwa na kupatikana baada ya saa 48, mtoto mwingine Idrissa Ally (13) ametekwa kwa mbinu za ‘kimafia’ na mtu asiyejulikana akiwa anacheza na wenzake.

Jumapili iliyopita, Beauty aliibwa akiwa katika Kanisa la FPCT Mbezi Mwisho, Dar es Salaam na alipatikana maeneo ya Kivule akiwa na msichana Angel Vincent (19) aliyedai kuwa mtoto huyo alikuwa wa shangazi yake.

Katika tukio jingine, Idrissa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Princes Gate, alichukuliwa juzi saa 11 jioni eneo la Tegeta Masaiti jijini hapa.
 
Akisimulia tukio hilo, mama wa mtoto huyo, Leila Kombe alisema Idrissa alirudi kutoka shuleni saa tisa alasiri kisha saa 10:30 jioni aliaga kuwa anakwenda kucheza na wenzake.

“Alitoka nyumbani na baiskeli akiwa amevaa fulana ya kijani na bukta ya rangi yenye mstari wa bluu, alikwenda moja kwa moja hadi nyumba ya tatu ambako kuna genge na alikutana na watoto wenzake,” alisema.

Mama Idrissa alieleza kuwa taarifa alizopewa na watoto waliokuwa naye, Idrissa alifika kwenye genge hilo linalouza bidhaa mbalimbali zikiwamo nyanya, vitunguu na matunda mbalimbali ambako mtoto wake huyo aliwaomba wenzake embe lakini walimtaka kwanza awape baiskeli waendeshe kuzunguka eneo hilo.
 
Back
Top Bottom