Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Idrissa alikubali na yeye alipewa embe akaanza kula, wakati akila ghafla lilitokea gari aina ya Toyota IST lenye rangi ya silver likaegeshwa karibu na genge hilo.

“Baadaye dereva mwanamume mwenye asili ya umanga (mwarabu) alishusha kioo na kuwasalimia watoto wale akiwamo mwanangu kwa kusema Asalaam Alaykum, Idrissa aliitikia Walaykum Salaam,” alisimulia mama huyo.

Alisema baada ya salaam, dereva huyo alianza kuzungumza na Idrissa kwa Kiingereza kabla ya kumuamuru aingie ndani ya gari lakini haikuwa kazi rahisi kwa kuwa hakukubali ombi hilo.
 
Kulikuwa na mabishano makali lakini mwishowe dereva yule aliwafukuza marafiki wa Idrissa na kutoa kichupa kidogo kinachodhaniwa ni ‘spray’ na kumpulizia mtoto wangu na hatimaye alimwingiza mlango wa nyuma wa gari lake,” alieleza.

Alisema ilipofika saa 12 jioni alisikia mlango ukigongwa akidhani ni mwanaye amerudi, kumbe walikuwa marafiki zake waliokuwa wakirudisha baiskeli.

“Nilikuwa nimemuandalia maji ya kuoga kwa sababu mwanangu ana tatizo la kifua na niliposikia hodi nikasema afadhali amerudi badala yake nakutana na baiskeli na kupewa taarifa za mwanangu kutoweka,” alisema mama huyo akiwa mwingi wa huzuni.
 
Nimechanganyikiwa, Idrissa ndio mwanangu wa kwanza. Wa pili anaitwa Ishati bado mdogo, tangu jana sijalala, sijui amepelekwa wapi mwanangu.”

Alisema eneo hilo limeanza kuwa tishio kwa usalama wa watoto kwani miezi miwili iliyopita, mtoto mwingine wa miaka mitatu anayeishi mtaa wa pili kutoka kwake, alichukuliwa na mtembea kwa miguu na alipatikana baada ya siku tatu huko Mwananyamala.
 
Mmoja wa watoto aliyekuwa na Idrissa, Shadrack Julius (9) alisema mtu huyo alipofika, alimkuta rafiki yake akila embe na kisha alitoa salaam na wakaanza kuzungumza Kiingereza.

“Baada ya kutoa salaam, tulisikia akimwita rafiki yetu kwa Kingereza ‘hey come here please’. Idrissa aligeuka na kujishika kifuani akijiuliza ni yeye. Yule dereva akajibu yes you (ndio wewe) Idrissa alisogelea lile gari na kuanza kuzungumza naye
 
Mmiliki wa genge hilo, Juvenile Bife ambaye hakuwapo wakati wa tukio hilo alisema taarifa alizopewa na mwanaye Lucy Yohana (13) ambaye alisema baada ya Idrissa kufika eneo hilo aliwaomba wenzake wampe embe na yeye alikubali kutoa baiskeli.

“Idrissa alitoa baiskeli lakini kwa masharti kuwa wasiende mbali kwa sababu kuna sehemu anataka kwenda.”

Kuhusu kuchukuliwa kwake, alisema baada ya dereva huyo kuzungumza na Idrissa hawakujua kilichoendelea na walidhani alikuwa anataka msaada.
 
Ally Iddi ambaye ni baba wa Idrissa, alisema kinachomsikitisha katika tukio hilo ni kwamba alimuona mwanaye wakati akienda gengeni kwa sababu ni maeneo ya karibu.

“Sikujua kama hili litatokea, alinipita nikiwa nimekaa na wenzangu, baada ya muda nikashangaa baiskeli ya Idrissa inaendeshwa na mtu mwingine, sikutilia shaka nikajua atakuwa amewapa marafiki zake kama kawaida ya watoto,” alisema Ally.

“Jambo hili limenishtusha sana sipo vizuri, kwa sasa. Binadamu kupotelewa na mtoto siyo jambo dogo, nimeshatoa taarifa Kituo cha Polisi Mbweni na kupewa RB namba WMB/BR/6947/2018,” alisema.
 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Princes Gate, Mussa Idrissa alisema ameshtushwa na taarifa za mwanafunzi wake kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.

“Asubuhi wakati nakuja kazini simu yangu ilianza kuita, kuangalia ni mama yake Idrissa sikupokea kwa sababu nilikuwa naendesha gari na sikujua kama kuna tatizo ila nilihisi school bus (basi la shule) halijaenda kumfuata mwanaye.

“Baada ya kufika shuleni dakika chache nikaona basi la shule likiingia, ghafla kondakta akaniambia kuwa hiyo simu uliyopigiwa na Mama Idrisa ni kwamba mwanaye ametekwa jana (juzi), nilishtuka, nikafunga safari kwenda nyumbani kwake,” alisema.
 
Baada ya kupata taarifa, alisema alianza kusambaza picha za mwanafunzi huyo katika makundi mbalimbali ya mitandao ya kijamii ambayo yanawajumuisha walimu wakuu na wasaidizi wa shule binafsi ili taarifa hizo zienee maeneo mbalimbali.

Alipoulizwa kuhusu tukio la kutekwa kwa mtoto huyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jumanne Murilo alisema kama wahusika wameshatoa taarifa kazi ya polisi ni kuzifuatilia ili kujua nini kilichotokea.
 
Kidomo domo kinaisha jumapili
FB_IMG_1538112626619.jpg
 
Back
Top Bottom