Ally Iddi ambaye ni baba wa Idrissa, alisema kinachomsikitisha katika tukio hilo ni kwamba alimuona mwanaye wakati akienda gengeni kwa sababu ni maeneo ya karibu.
“Sikujua kama hili litatokea, alinipita nikiwa nimekaa na wenzangu, baada ya muda nikashangaa baiskeli ya Idrissa inaendeshwa na mtu mwingine, sikutilia shaka nikajua atakuwa amewapa marafiki zake kama kawaida ya watoto,” alisema Ally.
“Jambo hili limenishtusha sana sipo vizuri, kwa sasa. Binadamu kupotelewa na mtoto siyo jambo dogo, nimeshatoa taarifa Kituo cha Polisi Mbweni na kupewa RB namba WMB/BR/6947/2018,” alisema.