Halafu kuna tangi jingine ambako humwaga mchanganyiko aliopata katika tangi la kwanza kisha anchunga bidhaa hiyo na matokeo yake ni karatasi anayotumia kutengeza kadi
‘Sasa hapa tunachunga kisha baadaye tunakausha huu mchanganyiko kwa jua, sasa hii ikikauka ndiyo inakuwa karatasia ambayo tunatumia kutengenezea kadi’
Michael ambaye alikosa ajira baada ya masomo yake ya shule ya upili, anasema alipata utalamu huu kutoka katika taasisi moja mjini Kisumu na amekuwa akifanya kazi hii kwa miaka mitatu sasa.
Kulingana naye wateja ni wachache lakini lengo lake ni kujenga kampuni ya karatasi akiamini kuwa hiyo ndiyo njia ya kumaliza gugumaji ziwa Victoria.